Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UAE mwachieni huru Alia Abdulnour aishi siku zake za mwisho akiwa huru-Wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

Wanawake wakimbizi wa ndani UAE wakijipanga kupokea msaada wa chakula kutoka Shirika la Msalaba mwekundu la UAE (Picha ya Maktaba)
UN/ Tobin Jones
Wanawake wakimbizi wa ndani UAE wakijipanga kupokea msaada wa chakula kutoka Shirika la Msalaba mwekundu la UAE (Picha ya Maktaba)

UAE mwachieni huru Alia Abdulnour aishi siku zake za mwisho akiwa huru-Wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

Haki za binadamu

Watalaamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa hii leo mjini Geneva Uswisi wamezisihi Falme za nchi za Kiarabu UAE kumwachia huru Alia Abdulnour, mwanamke ambaye kwa sasa anashikiliwa katika hospitali ya Tawam licha ya kwamba anasumbuliwa na saratani ya titi.

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR, inaripoti kuwa Bi Abdulnoor anashikiliwa katika chumba ambacho hakina madirisha wala matundu ya kupenyeza hewa na amefungwa kwa minyororo kwenye kitanda chake na akiwa chini ya ulinzi muda wote.

Bi. Abdnouralikamatwa na mamlaka za usalama tarehe 28 mwezi Julai  mwaka 2015 na akashitakiwa kwa madai ya kufadhili ugaidi baaada ya kuwa amesaidia kukusanya michango kwa ajili ya familia za wasyria walioko katika Falme za kiarabu pamona na wanawake na watoto walioko nchini Syria.

Wataalamu wamesema, “tuna wasiwasi mkubwa kuhusu hali yake ya kiafya upande wa mwili na akili na pia taarifa kuwa hali ya alikohifadhiwa kunamsababishia maumivu yasiyo na msingi.”

Kwa mujibu taarifa zilizopo, Bi Abdnour alishikiliwa katika kizuizi cha siri na katika eneo la peke yake pasipo kukutana na yeyote kwa kipindi cha miezi sita. Mwanamke huyo alikuwa akiteswa kimwili na kiakili katika kipindi chote hicho akipewa vitisho na kulazimishwa kupitia katika mateso makali ili akubali kukiri makossa kwa maandishi.

Wataaalamu wa Umoja wa Mataifa wameongeza kusema, “tunapenda kuwakumbusha UAE kuwa mateso na kumtendea mtu vibaya ni jambo ambalo halikubaliki duniani kote na kuwa tamko lolote au taarifa ya kukubali kosa baada ya mtu kuwa ameteswa, haiwezi kukubalika kama ushahidi.”

Falme za kiarabu
UN
Falme za kiarabu

Taarifa ya wataalamu wa haki za binadamu imeeleza pia kuwa saratani ya titi ainayomshambulia Bi. Abdulnouri mefikia katika hatua ya mwisho na kuwa sasa ugonjwa huo umeshaenea katika viungo muhimu vya mwili. Mwezo Novemba mwaka jana 2018 hali yake mbaya ilipozorota zaidi ndipo mamlaka zikampeleka katika hospital ya Mafraq.

Maombi yote yaliyofanywa na familia yake aachiwe ili apatiwe matibabu yalikataliwa na hatimaye alipozidiwa zaidi mnamo tarehe 10 mwezi uliopita wa Januari alihamishwa kutoka hospitali ya Mafraq akapelekwa Tawam iliyoko Al Ain ambako hata hivyo inadaiwa hapewi matibabu yanayofaa kumwondolea maumivu yanayomkabili.

“Tutawasiliana na mamlaka wamwachie huru Bi. Abdulnour na kumruhusu kuishi siku za mwisho za maisha yake kwa uhuru na akiwa na familia yake nyumbani. Pia tunatoa wito kwa serikali kuchunguza vitendo vya mateso na utendewaji mbaya anaodaiwa kufanyiwa mwanamke huyo na pia walioyatekeleza hayo wafikishwe wahukumiwe kwa mujibu wa sheria za kimataifa za haki za binadamu” wataalamu hao wamesema.