Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila ushirikiano wa kimataifa haki za binadamu itakuwa ndoto:UN

Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet (katikati kushoto) katika Baraza la haki za binadamu limeanza kikao chake cha 40 hii leo mjini Geneva UswisI
UN Photo/Violaine Martin
Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet (katikati kushoto) katika Baraza la haki za binadamu limeanza kikao chake cha 40 hii leo mjini Geneva UswisI

Bila ushirikiano wa kimataifa haki za binadamu itakuwa ndoto:UN

Haki za binadamu

Baraza la haki za binadamu limeanza kikao chake cha 40 hii leo mjini Geneva Uswis kikijadili juhudi za kitaifa na kimataifa katika kuchagiza na kulinda haki za binadamu. 

Katika kikao hicho cha ngazi ya juu kilichowaleta pamoja nchi wanachama na wadai wa haki za binadamu imesisitizwa pia umuhimu wa ushirikiano wa kimataoifa katika kushughulikia changamoto zilizoighubika dunia hivi sasa bna masuala yanayoleta walakini katika utimizaji haki za binadamu katika nchi na kanda mbalimbali duniani.

Akifungua kikao cha baraza hilo kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michele Bachelet amesema Haiwezekani kutimiza haki za binadamu endapo nchi zinaweka sera za maslahi yake mbele kuliko ya jamii na kutokuzingatia kutenda haki na kuongeza kwamba ambako viongozi wanaona mbali na kuona faida za kuwa na sera za haki za binadamu na utashi wa kisiasa kuzisongesha tutakuwa tayari kusaidia kuleta msaada wa vitendo kwani

(SAUTI YA MICHELLE BACHELET)

“Katika hali ya sasa , yenye mawimbi makubwa na misukosuko baharini, uongozi usio makini unaweza kuzitumbukiza nchi katika zahma, au tunaweza kutumia misingi ya haki kufikisha mashua yetu kwenye maji salama zaidi. 

Katibu Mkuu António Guterres (Picha ya maktaba)
Picha na UN/Jean-Marc Ferré
Katibu Mkuu António Guterres (Picha ya maktaba)

Akiunga mkono hilo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesisitiza

(SAUTI YA ANONIO GUTERRES)

“Kila mlango unaofungua ni fursa nyingine na kila haki unayotekeleza ni tofali lingine katika ujenzi wa dunia bora . Juhudi zenu zithibitoisha ni kwa kiasi gani haki za binadamu zinathamanini asilani hazipaswi kugeuzwa chombo. Na pia ni za muhimu katika kusongesha amani na utu, kuwawezesha wanawake na wasicha nan a kuleta matumaini.”

Pia amesema haki zilizoainishwa kwenye azimio la haki za binadamu ni za kila mtu na mahali popote, na haki hizo ziko huru bila kufungamana na utaifa, jinsia, mwenendo wa kimapenzi, rangI, dini , imani au hadhi yoyote. Amezitaka nchi zote kuzingatia hilo na kuhakikisha kila raia wake anafurahia na kutimiziwa haki zake.

Vitisho lazima vishughulikiwe:Espinosa

Hofu ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu migogoro na kutokuwepo utulivu imeainishwa pia na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakati wa kikao hicho Maria Fernanda Espinosa ambaye amesema “migogoro ya kiasiasa , na vita vinaweka vitisho vya wazi na ni lazima vishughulikiwe na kupatiwa dawa mujarabu na baraza hili na pia kutoka kwa mfumo mzima wa kimataifa kwa ajili ya ulinzi wa haki za binadamu.”

Pia Bi. Espinosa ameelezewa hofu yake kuhusu kuongezeka kwa pengo baiana ya walionacho na wasio nacho duniani.” Labda moja ya changamoto kubwa kwa ajenda ya haki za binadamu ni kutokuwepo kwa usawa , kujilimbikizia mali kumeongezeka kiasi kwamba mwaka 2018 watu binafsi 26 walikuwa na pesa zaidi ya masikini milioni 38 duniani.”

María Fernanda Espinosa Garcés;Rais wa kikao cha 73 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa , akizungumza wakati wa ufunguzi wa mjadala wa wazi wa Baraza hilo
Picha na UN/Cia Pak
María Fernanda Espinosa Garcés;Rais wa kikao cha 73 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa , akizungumza wakati wa ufunguzi wa mjadala wa wazi wa Baraza hilo

Haki za binadamu ni kitovu cha katiba iliyoanzisha UN

Viongozi wote kwenye kikao hicho wamesisitiza haja ya kukumbuka msingi wa kuundwa kwa Umoja wa Mataifa ambao ilikuwa ni haki za binadamu , na Katibu Mkuu Guterres amesema “Ilikuwa ni harakati za haki za binadamu na mafanikio ya wengine kote duniani ndizo zilizotufanya kuamini katika mabadiliko na kuhakikisha mabadiliko hayo yanayoteka, kwani haki za binadamu zinachagiza na kuwa chachu ya mabadiliko, na ukweli huo ndio muongozo wa Baraza hili, ni kitovu cha katiba ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa na ni muhimu kushughulikia changamoto zinazoikabili dunia yetu.

Hotuba za chuki zinazambaa kama moto wa nyikani

Umoja wa Mataifa unasema hotuba za chuki ni kinyume cha maadili ya demokrasia , utulivu wa kijamii na amani, na zinasambaa kama moto wa nyikani kupitia mitandao ya kijamii, intaneti na nadharia potufu zimejikita katika umma zikiwanyanyapaa wanawake, makundi ya walio wachache, wahamiaji na wakimbizi na wale wanaoitwa wengine. Na kwamba chuki hiyo inaelekea katika mfumo wa jamii iwe ni katika nchi zenye demokrasia ya wastan na hata katika tawala za kidikteta

Vipi chuki hiyo itatokomezwa

Ili kukata mizizi hiyo ya chuki Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametangaza kuanzishwa kwa mkakati wa haraka ili kuongeza juhudi za Umoja wa Mataifa za kukabiliana na hotoba za chuki na kuandaa mpango wa kimataifa wa kuchukua hatua ambao utaongozwa na mshauri maalumu wa Katibu Mkuu kwa ajili ya kuzia mauaji ya kimbari Adama Dieng.

Katibu Mkuu anasema “ni lazima kufufua tena utu wa kimataifa kwa ajili ya ulinzi wa wakimbizi na kuendelea kufanya kazi kwa ajili ya maadili na ushirikiano wa kimataifa katika kurejesha haki na kusaidia kuwalinda watu dhidi ya wasafirishaji haramu wa binadamu, na wahalifu wahalifu wengine. Kikao hiki cha Baraza la haki za binadamu kitaendelea hadi Machi 22.