Mamlaka Venezuela msitumie silaha za sumu dhidi ya waandamanaji- Guterres

22 Februari 2019

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo amekuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela, Jorge Arreaza, ambapo amesisitiza tena kuwa hatua zozote ambazo chombo hicho kitachukua kusaidia wahitaji nchini Venezuela zitazingatia kanuni na misingi ya kibinadamu, kutoegemea upande wowote na mamlaka za taifa hilo na kushirikiana na taasisi za taifa hilo.
 

Hii ni mara ya tatu ndani ya wiki chache kwa viongozi hao kukutana tangu kuanza sakata nchini Venezuela kati ya Rais Nicolas Maduro na mpizani wake Juan Guaidó.

Taarifa ya msemaji wa Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo jijini New York, Marekani, imesema katika mkutano wao wa leo kwenye makao makuu ya umoja huo wawili hao wamejadili hali inavyoendelea nchini Venezuela, kwenye ukanda wa Amerika ya ku ambapo Bwana Guterres amesihi mamlaka za Venezuela ziache kutumia silaha za sumu dhidi ya waandamanaji ambao wanapinga serikali ya Rais Maduro.

Huku mustakabali wa hali ya kiuchumi na kisiasa ukiwa mashakani, Umoja wa Mataifa umekuwa ukisaidia taasisi za nchini humo kupatia wanawake na watoto vikasha vya dawa muhimu na watoa huduma za misaada wamesambaza huduma dhidi ya unyafuzi kwa watu 100,000.

UNHCR/Santiago Escobar-Jaramillo
Wakimbizi na wahamiaji kutoka Venezuela wakivuka mpaka kuingia Comombia mnamo tarehe 16 Oktoba 2018

Umoja wa Mataifa unasema makazi Sita ya muda yameanzishwa kwenye majimbo ya mpakani mwa magharibi mwa Venezuela na yanapatia makazi watu 1,600 sambamba na huduma ya taarifa za ulinzi na usalama na vikasha vya kifamilia vilivyosheheni chakula na mavazi.

Nalo shirika la afya ulimwenguni, WHO limethibitisha kuwa linaendelea kushirikiana na mamlaka za Venezuela kupitia shirika la afya kwa nchi za Amerika, PAHO ili kuzuia na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.

Tayari kampeni za chanjo zimeanza ili kukomesah kuenea kwa ugonjwa wa surau na dondakoo.
Katika kuhakikisha inaweza kusaidia wavenezuala milioni 3.6 wakiwemo watoto milioni 2,  ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA tayari imeomba tarkibani dola milioni 110.

 

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter

Fuatilia Habari: Habari zilizopita za Mada Hii

Fahamu kwa kina msimamo wa UN na sakata la Venezuela

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza wasiwasi wake kuhusu hali inayoendelea hivi sasa nchini Venezuela ambako kuna mvutano kati ya serikali ya Rais Nicolas Maduros na kiongozi wa upinzani Juan Guaidó.

Sakata la Venezuela: Katibu Mkuu hana mamlaka ya kutambua au kutotambua taifa au kiongozi wake- Dujarric

Wakati vuta nikuvute ikiendelea nchini Venezuela kati ya Rais Nicolas Maduros na Juan Guaidó aliyejitangaza kuwa rais wa nchi hiyo, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema kuwa Katibu Mkuu hana mamlaka ya kueleza kukubali au kukataa nchi mwanachama au kiongozi wake.