Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna ongezeko la visa vya surua kote ulimwenguni-WHO

Mtoto akipatiwa chanjo dhidi ya surua nchini Paraguay
Picha:WHO/PAHO
Mtoto akipatiwa chanjo dhidi ya surua nchini Paraguay

Kuna ongezeko la visa vya surua kote ulimwenguni-WHO

Afya

Takwimu za Shirika la afya ulimwenguni, WHO zinaonyesha kuwa idadi ya maambukizi ya surua inaongezeka katika maeneo mabli mbali na sio changamoto ya bara moja

WHO imesema mlipuko wa surua sehemu moja ni changamoto kwa wote. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi  Mkurugenzi wa kitengo cha utaoji chanjo kwenye shirika la WHO, Katherine O’Brien amesema kunashuhudiwa milipuko ya muda mrefu, mikubwa na ambayo inaendelea kusambaa.

Kwa mujibu wa takwimu za WHO kwa mwaka 2018 hadi katikati ya mwezi Januari mwaka huu kuliripotiwa visa 229,068 duniani kote ambapo barani Afrika kuliripotiwa visa 33,879   ambapo miongoni mwa visa hivyo  4,391ni kutoka Madagascar, Marekani na Amerika Kusini visa, 16,966, Mediteranea mahsariki 21,905, na bara Ulaya visa 59,578.

WHO imeongeza kuwa surua ni ugonjwa ambao unaweza kuzuilika kwa kupokea chanjo na kwamba mabilioni ya watoto hupokea chanjo dhidi ya ugonjwa huo unaoambukiza kwa njia ya hewa.

 Bi O’ Brien amesema surua ni ugonjwa unaombukiza kupitia virusi na husababisha, homa, vipele na madhara mengine ikiwemo kuvimba kwa ubongo, h upofu, nimonia, na hata vifo.

Shirika hilo la afya limesisitiza kuwa chanjo dhidi ya surua ni salama na madai kwamba chanjo hiyo inasababisha usonji haina mashiko kwani ni uvuumi ambao umethibitishwa si kweli. Chanjo dhidi ya surua na huzuia ugonjwa huo lakini wakati mwingine inatokea virusi hivyo vinaambukiza sana na iwapo mtu mmoja ameugua surua basi a watu  watu wengine tisa hadi kumi watapata maambukizi ya ugonjwa huo kama hawana kinga na kwa sababu inaambukiza kwa njia ya hewa basi virusi vyake vinaweza kusambaa kwa urahisi zaidi.

 Mkurugenzi huyo amesema hali inayoshuhudiwa inatokana na kutochanja na sio ukosefu wa chanjo. Kila mtoto anahitaji kupokea dozi mbili za chanjo dhidi ya surua.