Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta ya mifugo yaweza kuwa dawa mujarabu ya kutokomeza njaa-FAO

Kundi la ng'ombe malishoni karibu na kijiji huko Kazakhstan
Daniil Nenashev/World Bank
Kundi la ng'ombe malishoni karibu na kijiji huko Kazakhstan

Sekta ya mifugo yaweza kuwa dawa mujarabu ya kutokomeza njaa-FAO

Ukuaji wa Kiuchumi

Sekta ya mifugo ni miongoni mwa wachangiaji wakubwa wa ongezeko la joto duniani  hasa wakati huu idadi ya watu ikiongezeka na watu hao wakihitaji kulishwa, shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo , FAO  inasema sekta hiyo inaweza kuwa suluhu badala ya tatizo. 

Kwa miaka nenda miaka rudi   licha ya umuhimu na faida za sekta ya mifugo imekuwa ikibebeshwa lawana ya kuchangia hasa hewa ya ukaa . Na je sekta hiyo inaweza kubadilika kutoka kuwa sehemu ya tatizo na kuwa sehemu ya suluhu? Kwa mujibu wa Heinning Steifield mkuu wa kitengo cha mifugo, utafiti na será wa FAO inawezekana na kwamba

(Sauti ya Heinning )

“Sekta ya mifugo inachangia katika lengo la kutokomeza njaa kwa kuwa muhimili wa maisha kwa wafugaji wengi na wakulima wadogowadogo, mamilioni wanategemea mifugo kwa maisha yao , inatoa moja kwa moja chakula, inatoa kipato na muhimu zaidi inachangia fedha za kununulia chakula, inatoa aina kubwa ya  mtaji kwa wafugaji na wakulima wadogowadogo kwa kuwa na mifugo, na inawapa utulivu katika maisha ambao bila mifugo wasingekuwa nao.”

Hata hivyo anasema linapokuja sula la kuibadili sekta hiyo ingawa unawewzekana lakini sio kazi ya rahisi.

(Sauti ya Heinning )

"Itakuwa vigumu lakini tayari tumebaini aina mbalimbali za mitazamo ambayo itatusaidia kufanya hivyo. Tunajua kwamba kupitia kuboresha uzalishaji tunaweza kupunguza utoaji wa hewa chafuzi katika baadhi ya maeneo, na pia tunafahamu kwamba baadhi ya taka za bidhaa za  uchumi utokanao na mifugo zinaweza kutumika tena kutengeneza vitu kama chakula cha kulisha mifugo badala ya kuzalisha kingine.”