Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lishe bora ni haki ya kila mtoto:UNICEF

Chakula chenye virutubisho vya kutosha vya lishe kinaweza kumwondoa mtu hususani watoto katika hatari ya kupata magonjwa.
World Bank/Maria Fleischmann
Chakula chenye virutubisho vya kutosha vya lishe kinaweza kumwondoa mtu hususani watoto katika hatari ya kupata magonjwa.

Lishe bora ni haki ya kila mtoto:UNICEF

Haki za binadamu

Lishe bora na huduma zingine za msingi kama elimu na afya ni haki ya kila mtoto kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, lakini mara nyingi mamilioni ya watoto hukosa haki hiyo hususani lishe bora kutokana na sababu mbalimbali. UNICEF inasema hali hiyo  inaweka afya za watoto hatarini na pia njiapanda mustakhbali wao.

Mkoani Ruvuma nchini Tanzania kuna watoto walioathirika na utapia mlo kwa kukosa lishe bora, lakini wengine hata kushindwa kuhuduria masomo  kwa sababu hiyo. John Kabambala kutoka Radio washirika Tanzania Kids FM alitembelea shule ya msingi Gracious ya mjini Songea mkoani humo kupata maoni ya waalimu na wanafunzi kuhusu haki ya lishe bora kwa watoto na jukumu la wazazi kuhakikisha haki hiyo inatimia.

Mwalimu  Estina Msigwa anasema  kuna wazazi ambao  wanajipendelea zaidi kuliko watoto wao kwa kula vyakula ambavyo ni vizuri kuliko vile wanavyowapatia watoto wao ingawa anaamini kuna wale ambao hawawalishi watoto wao vizuri kulingana na hali ya kipato. Mawazo yake yanaungwa mkono na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo  Jaredi   Misinze anayesema, “ kuwanyima Watoto chakula kizuri ni kuwanyima watoto haki. Watoto wana haki zote za kupata chakula kizxuri ambacho wao wazazi wenyewe wanapenda kula”