Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka minne iliyopita ilikuwa na viwango vya juu vya joto kuwahi kushuhudiwa- WMO

Katika picha hii ya mwaka 2016 iliypigwa kwenye kijiji cha Siyephi Wilaya ya Bullilima jimbo la Matebele kusini nchini Zimbabwe, ni msichana wa akiwa amesimama katika bwawa linalokauka, eneo yeye na familia yake walikokuwa wakiteka maji.
UNICEF/Mukwazhi
Katika picha hii ya mwaka 2016 iliypigwa kwenye kijiji cha Siyephi Wilaya ya Bullilima jimbo la Matebele kusini nchini Zimbabwe, ni msichana wa akiwa amesimama katika bwawa linalokauka, eneo yeye na familia yake walikokuwa wakiteka maji.

Miaka minne iliyopita ilikuwa na viwango vya juu vya joto kuwahi kushuhudiwa- WMO

Tabianchi na mazingira

Shirika la hali ya hewa duniani, WMO limesema ongezeko la viwango vya joto ni ishara dhahiri ya mabadiliko ya tabianchi ya muda mrefu, huku ikisema miaka minne iliyopita viwango vilikuwa vya kipekee.

WMO katika taarifa iliyochapishwa kwenye wavuti wake imesema miaka  ya 2015, 2016, 2017 na 2018 imekuwa ya joto zaidi ikisema kuwa ni “ishara dhahiri kuwa mabadiliko ya tabianchi yanaendelea.”

Uchambuzi wa WMO  unaonyesha kuwa kiwango vya wastani vya nyuzi joto kwa vipimo vya selsiasi kilikuwa ni 1,0 juu ya viwango vya kabla ya miaka ya kuanzishwa kwa viwanda 1850 hadi 1900.

Mwenendo wa muda mrefu

Akizungumzia mwenendo wa hali ya hewa, Katibu Mkuu wa WMO, Petteri Taalas amesema mwenendo wa muda mrefu ni muhimu kuliko kuangalia mwaka mmoja mmoja na kwamba taswira inaonyesha kuwa viwango vya joto vinapanda akisema, “miaka 20 iliyo na joto zaidi imekuwa miaka 22 iliyopita. Viwango vya joto katika kipindi cha miaka minne iliyopita vimekuwa vya aina yake nje na ndani ya bahari".

Bwana Taalas amesema viwango vya joto ni kiungo tu kwenye taswira  kwani  athari  kubwa na mbaya zitokanazo na hali ya hewa viliathiri nchi nyingi na mamilioni ya watu na kusababisha athari mbaya kwenye uchumi na mazingira mwaka 2018.

Mabadiliko ya tabianchi

Kwa mujibu wa WMO, matukio mengi ya hali ya hewa yanaambatana na matokeo ya moja kwa moja ya mabadilko ya tabianchi na hivyo ni muhimu kukabiliana na hali halisi. 

Kwa mantiki hiyo bwana Taalas, amesema kupunguza gesi chafuzi na kuweka mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi vinapaswa kuwa vipaumbele kimataifa.

Viwango vya joto kwa mwaka 2018 vilikuwa kwa wastani wa nyuzi joto 0.38 katika kipimo cha selsiyasi, juu ya vipimo vya kati ya 1981 hadi 2010 vya wastani vilivyokadiriwa kuwa 14.3