Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamert asisitiza umuhimu wa kuheshimu mkataba wa kusitisha uhasama Hodeidah

Meli Amity ikiwa imetia nanga katika bandari ya Hudeidah Yemen. bandari hiyo ndiyo msaada karibu wote kwa yemen hupitia.
WFP/Fares Khoailed
Meli Amity ikiwa imetia nanga katika bandari ya Hudeidah Yemen. bandari hiyo ndiyo msaada karibu wote kwa yemen hupitia.

Kamert asisitiza umuhimu wa kuheshimu mkataba wa kusitisha uhasama Hodeidah

Amani na Usalama

Kamati ya kuratibu mchakato wa kuondoa vikosi inayoongozwa na jenerali Patrick Camert, imefanya mkutano wake wa tatu leo Jumapili ndani ya meli ya Umoja wa Mataifa kwenye bandari ya Hodeidah, ukijumuisha wawakilishi wa serikali ya Yemen na wa Ansar Allah (wa Houthi)

Kamert ameanza mkutano kwa kusisitiza umuhimu wa kuheshimu mkataba wa kusitisha mapigano ulioanza kutekelezwa Disemba 18. Amezionya pande zote kuhusu unyeti wa mkataba huo na kuwataka wawaamuru viongozi wao kwenye maeneo husika kujizuia na ukiukwaji zaidi wowote ambao utahatarisha makubaliano ya Stockholm na mchakato mzima wa amani.

Pande zote mbili zimehakikisha dhamira yao ya kutekeleza makubaliano ya Amani ya Stockholm kwa ajili ya Hodeidah  na hususan dhamira yao ya kusaka suluhu ambayo itafungua njia ya Hodeidah-Sanaa ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kwenda kwenye vinu vya bahari ya shamu.

Mazungumzo hayo yaliyokuwa ya muhimu nay a kujenga yamepangwa kuendelea tena kesho Jumatatu.

Pande husika ambazo ni serikali ya Yemen na Ansar Allah (wa Houthi) waliafikiana majadiliano kwenye mkutano wa mwaka jana nchini Sweeden kuondoa vikosi kwenye bandari za Hodeidah, Salif, Ras Issa na Hodeidah kwenda kwenye eneo waliloafikiana nje ya mji na bandari.