Tuunge mkono utekelezaji makubaliano ya amani yaliyofikiwa na CAR:UN

2 Februari 2019

Baada ya majadiliano ya siku 10 mjini Khartoum nchini Sudan, serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR na makundi 14 yenye sialaha hatimaye leo Jumamosi wamefikia muafaka wa amani , kwa mujibu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini CAR wa MINUSCA.

Kupitia mtandao wake wa twitter MINUSCA imesema makubaliano hayo yamewezekana chini ya mradi wa Afrika kwa ajili ya amani na maridhiano kwa taifa la CAR ulioongozwa na Muungano wa Afrika, AU kama mpatanishi kwa msaada mkuwa wa Umoja wa Mataifa.

Akizungumzia hatua hiyo kubwa mkuu wa opereshini za ulinzi wa Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix amesema kwenye mtandao wake wa twitter amesema  “Na hebu tushikamane tuunge mkono utekelezaji wa makubaliano haya ya amani”  baada ya tangazo la hitimisho la makubaliano hayo kufikiwa kwenye mji mkuu wa Sudan. 

Naye afisa wa Muungano wa Afrika balozi Smail Chergui ambaye ni Kamishina wa tume ya AU kwa ajili ya amani na usalama , amesema “hii ni siku nzuri sana na muhimu kwa CAR na watu wake wote “na amezitaka pande zote za nchi hiyo kuunga mkono makubaliano haya akiongeza kuwa “yatawezesha watu wa CAR kufuata njia ya maridhiano , umoja na maendeleo.” Pia ameushukuru Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika Au kwa mchango wao kufanikisha makubaliano hayo

Baaba ya makubaliano hayo Jumamosi ambayo yalimtia matumaini Bwana Chergui baada ya kuona pande kinzani sinaingia kwenye majadiliano kwa mara ya kwanza kwa dhamira ya kupata muafaka. Kamishina huyo amesisitiza ushirikiano ambao ni mfano kwa pande zote.

Naye kiongozi wa ujumbe wa serikali ya CAR kwenye mazungumzo hayo mjini Khartoum , Firmin Ngrebad amesema amedhamiria “kufanyakazi na kiongozi wa nchi na serikali yake kutekeleza masuala yanayotiliwa Mashaka na kaka zetu walioamua kubeba silaha.”

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud