Baraza la Usalama liko tayari kusaidia kufanikisha kazi za mjumbe wa Sahara Magharibi

31 Januari 2019

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wameelezea mshikamano wao na mjumbe binafsi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Sahara Magharibi, Horst Köhler ambaye ni rais wa zamani wa Ujerumani.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambapo wajumbe wa Baraza hilo wamekaribisha hotuba ya mjumbe huyo na kuelezea utayari wao kumuunga mkono kwa ajili ya kutimiza wajibu wake.

Kwa kuzingatia azimio 2440 la mwaka 2018, wajumbe hao wa Baraza la Usalama wamekaribisha ushiriki wa Morocco, kundi la Frente Polisario, Algeria na Mauritania katika majadiliano ya pamoja ya Desemba5-6, 2018, wametambua dhamira yao ya kushiriki katika majadiliano ya pamoja kwa mara ya pili katika robo ya kwanza ya mwaka 2019 na wameelezea msaada wao katika mchakato mzima nanafasi ya mjumbe binafsi.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter