Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makaburi ya pamoja yabainika huko DRC

Walinda amani wa MONUSCO nchini Congo DRC, wakifanya doria mjini Butembo Januari 2019.
MONUSCO
Walinda amani wa MONUSCO nchini Congo DRC, wakifanya doria mjini Butembo Januari 2019.

Makaburi ya pamoja yabainika huko DRC

Haki za binadamu

Zaidi ya makaburi 50 ya pamoja nay a mtu mmoja mmoja yamebainika kwenye eneo la Yumbi, jimbo la Mai-Ndombe nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kufuatia mauaji yaliyoripotiwa kwenye eneo  hilo  katikati ya mwezi uliopita wa Disemba. 

Mkurugenzi wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini DR Congo, Abdul Aziz Thioye amesema hayo baada ya kutembelea eneo la Yumbi, kufuatia ziara iliyoandaliwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO.

Yumbi ni moja ya maeneo yenye vikundi vilivyojihami ambako hata uchaguzi mkuu uliahirishwa kutokana na ukosefu wa usalama. Akizungumzia walichoshuhudia kwenye eneo hilo la Yumbi lililokuwa kitovu cha mapigano, Bwana Thioye amesema,

(Sauti ya Abdul Aziz Thioye)

"Kuna takribani makaburi 50 yaliyozika watu wengi na pia ya mtu mmoja mmoja ambayo tumegundua. Hii inadokeza kuwa idadi ni kubwa. Kaburi la pamoja kulingana na ukubwa wake, linaweza kuwa na maiti watano hadi 10, na kwa urefu inaweza kuwa 100 hadi zaidi.”

Ofisi ya haki za binadamu imesema mapigano kati ya kabila la Batende na Banunu yalisababisha watu 890 kuuawa kati ya tarehe 16 na 18 mwezi uliopita wa Disemba kwenye vijiji vinne huko Yumbi.

Hata hivyo kaimu mtawala kwenye enoe hilo anasema idadi ya waliouawa ni zaidi ya 500.