Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zahma Kaskazini mwa Nigeria yahitaji zaidi ya dola milioni 800 kuikabili kwa 2019-2021:UN

Wakikmbizi wa Nigeria wakiondoka katika kambi ya Ngouboua katika ufukwe wa ziwa Chad. Picha hii ilipigwa Februari 2015
UNHCR/Olivier Laban-Mattei
Wakikmbizi wa Nigeria wakiondoka katika kambi ya Ngouboua katika ufukwe wa ziwa Chad. Picha hii ilipigwa Februari 2015

Zahma Kaskazini mwa Nigeria yahitaji zaidi ya dola milioni 800 kuikabili kwa 2019-2021:UN

Msaada wa Kibinadamu

Mamilioni ya raia wanaendelea kuteseka na hali ngumu Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na eneo zima la Bonde la ziwa Chad ambako machafuko ya karibuni yamesababisha maelfu mengine ya watu kufungasha virago na kuongeza madhila katika hali ya kibinadamu ambayo tayari ilikuwa mbaya.  

Ili kukabiliana na hali hiyo ya kibinadamu Umoja wa Mataifa na wadau kwa kuisaidia serikali ya Nigeria na nchi zinazohifadhi  maelfu ya wakimbizi wa Nigeria, leo wamezindua  ombi la mkakati wa kibinadamu na masaada kwa wakimbizi kwa ajili ya mwaka 2019-2021.

Ombi hili linahitaji dola milioni 848 na nyongeza ya dola milioni 135 kwa ajili ya wakimbizi ili kuweza kuendelea kutoa msaada wa chakula, maji , malazi na ulinzi kwa maelfu ya raia wa Nigeria na nchi za jirani za Cameroon, Chad na Niger. Akifafanua kuhusu ombi hilo msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA, Jens Learke amesema mashirika ya misaada yamedhamiria kuwafikiwa watu milioni 6.2 mwaka huu ambao wameathirika vibaya na machafuko ya Kaskazini Mashariki mwa Nigeria ambayo sasa yamedumu kwa mwaka wa 10. Wengi wa watu hao wanakabiliwa na njaa, maelfu ya watoto wanautapia mlo, na maelfu hawasomi hususan katika majimbo ya Borno, Adamawa na Yobe , hivyo Jens Learke anasema, “Mkakati huu unalenga kushughulikia mahitaji haya ya haraka. Msaada wa chakula pekee unachukua karibu theluthi ya fedha zinazohitajika, yakifuatiwa na lishe, afuya,na maji na miradi ya usafi. Karibu dola miliini 50 zinahitajika kwa ajili ya elimu ya dharura.”

Ameongeza kuwa ukosefu wa usalama na vitisho vya mashambulizi vimeendelea kuwa changamoto kubwa ya utoaji huduma za kibinadamu. Ombi la leo limetolewa kwa ushirikiano wa OCHA, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo , UNDP na serikali ya Nigeria.