Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres atoa wito dunia kuweka elimu kama kipaumbele ili kufikia malengo ya SDGs

Kwa kuanzishwa Chuo hicho Kikuu cha Turkana, Esther Nyakong mwenye umri wa miaka 17 kutoka nchini Sudan Kusini, ataweza kuendelea na masomo yake ya elimu ya juu.
UNHCR/Benjamin
Kwa kuanzishwa Chuo hicho Kikuu cha Turkana, Esther Nyakong mwenye umri wa miaka 17 kutoka nchini Sudan Kusini, ataweza kuendelea na masomo yake ya elimu ya juu.

Guterres atoa wito dunia kuweka elimu kama kipaumbele ili kufikia malengo ya SDGs

Utamaduni na Elimu

Wakati dunia ikiadhimisha siku ya kimataifa ya elimu kwa mara ya kwanza hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres katika ujumbe wake kwa siku hii amesema, elimu hubadilisha maisha.

Katibu Mkuu amemnukuu balozi mwema wa amani wa Umoja wa Mataifa Malala Yousafzai ambaye alisema, “mtoto mmoja, mwalimu mmoja, kitabu kimoja, na kalamu moja vinaweza kubadili ulimwengu.” Na Nelson Mandela na ujumbe wake ambapo alisema elimu ni “silaha kubwa zaidi ambayo unaweza kutumia kubadili ulimwengu.”

Akirejelea miaka yake ya awali kabla ya kuhudumu kwenye Umoja wa Mataifa au ofisi ya umma, Bwana Guterres amesema alikuwa mwalimu katika maeneo ya vitongoji duni Lisbon ambako amesema, “nilishuhudia kuwa elimu ni injini ya kutokomeza umaskini na nguvy ya Amani”.

Katibu huyo Mkuu amesema, leo elimu ni kiini cha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs na kwamba dunia inahitaji elimu kumaliza kutokuwepo usawa na kuimarisha afya, kufikia usawa wa kijinsia na kutokomeza ndoa za utotoni na kulinda raslimali za sayari dunia. Aidha ameongeza kuwa tunahitaji elimu kukabiliana na hotuba za chuki, chuki dhidi ya wageni, kutovumiliana na kujenga uraia wa kimataifa.

Mradi wa dharura kwa elimu ulio chini ya shirika la UN la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA husaidia pia kampeni ya mwaka ya watoto kurejea shule muhula mpya wa masomo unapoanza mwezi Septemba.
UNRWA/Rushdi El-Saraaj
Mradi wa dharura kwa elimu ulio chini ya shirika la UN la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA husaidia pia kampeni ya mwaka ya watoto kurejea shule muhula mpya wa masomo unapoanza mwezi Septemba.

Kwa sasa watoto milioni 262 hawahudhurii shule, barubaru na vijana hawapo shuleni, idadi kubwa yao ni wasichana na mamilioni wanaohudhuria shule hawapati stadi za msingi.

Bwana Guterres ametaja hali hiyo kuwa ni ukiukwaji wa haki ya elimu ambapo amesema dunia haiweza kusonga mbele iwapo ina watoto na vijana ambao hawana stadi zinazohitajika kushindana katika soko ya ajira kwenye karne ya 21, na hatuwezi kuwacha nusu ya binadamu nyuma.

Kwa mantiki hiyo Guterres amesema ni lazima kuongeza juhudi kusongesha SDG4 mbele kuhakikisha elimu jumuishi na sawa na kuchagiza fursa za kusoma za muda mrefu kwa wote.

Akirejelea mabadiliko yanayoweza kufikiwa kwa kuimarsha elimu, Katibu Mkuu amesema elimu inaweza kuvunja minyororo ya umaskini kwani utafiti unaonyesha kuwa iwapo watoto wa kike na kiume wakimaliza sekondari, watu milioni 420 wanawazu kuepukana na umaskini.

Hivyo ametoa wito kwa dunia kuweka elimu kama kipaumbele, kuiunga mkono kwa ushirikiano na ufadhili na kutambua kuwa kutoacha mtu yeyote nyuma kunaanza na elimu.

 

TAGS: Elimu, siku ya elimu duniani, Antonio Guterres