Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchakato wa amani Colombia unahitaji kuungwa mkono- Massieu

Wanawake na watoto kutoka jamii ya Mocoa nchini Colombia wakiwa wakiwasha mishumaa kuandika neno amani, amani ambayo wanalilia kwenye eneo lao.
UNHCR/Ruben Salgado Escudero
Wanawake na watoto kutoka jamii ya Mocoa nchini Colombia wakiwa wakiwasha mishumaa kuandika neno amani, amani ambayo wanalilia kwenye eneo lao.

Mchakato wa amani Colombia unahitaji kuungwa mkono- Massieu

Amani na Usalama

Miaka miwili baada ya kutia saini makubaliano ya amani nchini Colombia na kisha kufuatia ongezeko la ghasia nchini humo, wananchi wamezindua mikakati ya kufikia maridhiano ya ujumla.

Hiyo ni kwa mujibu wa mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Carlos Ruiz Massieu wakati akihutubia Baraza la Usalama, hii leo kuwa huku akisisitiza hatua za kuchukua ili kuweka utulivu nchini humo.

Hotuba ya Carlos Ruiz Massieu kwa Baraza la Usalama imekuja siku chache baada ya shambulio kwenye Chuo cha Polisi kwenye mji mkuu wa Colombia, Bogotá ambapo watu 21 waliuawa na makumi wengine wamejeruhiwa ambapo kundi la National Liberation Army (ELN) lilidai kutekeleza ugaidi huo.

Kwa jumla watu 220,000 wameawa tangu kuanza kwa mzozo huo mwaka 1964, kati ya vikosi vya serikali na vikundi vilivyojihami vya waasi kubwa ikiwa ni kundi la waasi la FARC na wauza madawa ya kulevya.

“Katika hatua ya kukataa  shambulio hilo wanasiasa nchini Colombia na watu waliandamana nchini humo Jumapili, raia wakionyesha kutokubaliana na ukatili,” amesema Ruiz Massieu ambaye aliteuliwa tarehe 7 mewzi huu kusimamia utekelezaji wa makubaliano ya amani ya Novemba 2016. Ameongeza kuwa, “makubaliano hayo lazima yaendelee kupaliliwa”.

Hatua kubwa kuelekea maridhiano

Mwakilishi huyo maalum alikwenda mbali zaidi kuelezea baadhi ya hatua zilizopigwa katika kutekeleza makubaliano ya amani, ikiwemo kuteuliwa kwa jopo la ngazi ya juu la serikali kuhusu jinsia linalolenga kutekeleza makubaliano kuhusu jinsia kwa mujibu wa makubaliano ya amani walikutana kwa mara ya kwanza Januari 16 mwaka huu.

Aidha ametaja hatua muhimu ya kuanzishwa kwa kamisheni ya ukweli mwezi Mei mwaka 2018 iliyobuniwa kwa ajili ya kuangalia ukiukaji wa haki za binadamu ikiwemo ukatili wa kingono na kuimarisha maridhiano katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Carlos Ruiz Massieu, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UN Colombia akihutubia Baraza la Usalama Januari 23, 2019
UN/Eskinder Debebe
Carlos Ruiz Massieu, Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UN Colombia akihutubia Baraza la Usalama Januari 23, 2019

Bwana Massieu amesema kuwa mamlaka inayosimamia amani inayoamua kuhusu ukatili ualiotekelezwa wakati wa mzozo wa makundi yaliyojihami na iliyoanza kufanya kazi mwaka mmoja uliopita kwas asa unatathmini kesi tano za matukio ya kikatili yaliyoathiri takriban watu 32,000.

“Kama Baraza lilivyosisitiza, inasalia muhimu kwamba mamlaka hiyo maalum iwe huru na ijisimamie na kwamba itapata msaada inayohitaji ili kutekeleza majukumu yake kama ipasavyo,” amesema mwakilishi huyo maalum.

Ujumuishwaji na usalama

Bwana Massieu ametaja changamoto zilizopo kuwa “ni pengo katika ujumuishwaji kiuchumi waasi ikiwemo wa kikundi cha FARC. Ameongeza kuwa baadhi ya mikutano mashinani imeonyesha nia kubwa ya waasi kufanya kazi na kurejelezkatika maisha ya kawaida katika jamii na kwamba wana wasiwasi kuhusu usalama wao ikiwemo usalama kisheria na mustakabali wao kiuchumi.”

Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa inapendekeza kuwa  juhudi laima ziongezwe kasi kuwezesha umiliki wa ardhi na kuendeleza soko za bidhaa na huduma zinazozalishwa.

Katika hatua ya kujumuisha  na kuleta mabadiliko ya kisiasa FARC itashiriki kwenye uchaguzi, Oktoba 27 mwaka huu ambapo juhudi zinafanyika kuhakikisha usalama na ulinzi wa vyama vyote.

Nchini Colombia hali ya kiusalama bado ni dhaifu kwa mujibu wa ripoti ya Katibu Mkuu huku ofisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu ikisema tangu kutiwa saini makubaliano ya amani mwaka 2016, watu 163 ya viongozi wa jamii na watetezi wa haki za binadamu yamethibitishwa na vifo takriban 454 vimeripotiwa. 

Katika wiki ya kwanza ya mwezi huu pekee, viongozi saba wameuawa na takriban mashambulizi 31 yameripotiwa ambapo wafuasi wa FARC wakati mwingi ndio walengwa, jambo ambalo limeelezwa ni changamoto kwa maridhiano ya kitaifa.

Bwana Massieu amesema usalama wa viongozi na wanachama wa FARC unaendana na uwezo wa mamlaka kuhakikisha usalama jumuishi unaozingatia uwepo wa vikosi vya usalama na raia katika maeneo kunakoshuhudiwa mizozo.

Mwakilishi maalum huyo amesisitiza kuwa moja ya ujumbe mkuu ambao amesikia kutoka kwa wacolombia wakati wa ziara yake mashinani, ni kwa jinsi gani wanakaribisha na kutarajia msaada wa jamii ya kimataifa wakati wakijitahidi kukabiliana na changamoto nyingi ili kufikia amani.

Aidha ameongeza kuwa ushirkiano na msaada wa Baraza la Usalama utasalia kuwa kiungo muhimu katika mchakato wa amani.