Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guatemala: Mabadiliko katika sheria ya maridhiano huenda ikasamehe wahalifu wa ukatili dhidi ya binadamu

Hifadhi ya wahanga wa mauaji na waliotoweshwa ya nchini Guatemala.(maktaba)
UNDP Guatemala/Caroline Trutmann Marconi
Hifadhi ya wahanga wa mauaji na waliotoweshwa ya nchini Guatemala.(maktaba)

Guatemala: Mabadiliko katika sheria ya maridhiano huenda ikasamehe wahalifu wa ukatili dhidi ya binadamu

Haki za binadamu

Kamishna mkuu wa haki za binadamu, wa Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet leo ameelezea wasiwasi wake kuhusu kusomwa kwa mara ya kwanza ndani ya bunge la nchi hiyo, kwa muswada wa kubadili sheria kuhusu maridhiano nchini Guatemala.

Muswada huo iwapo utapitishwa utamaanisha msamaha kwa kesi zote dhidi ya haki za binadamu na uhalifu uliotekelezwa wakati wa mzozo wa miongo uliohusisha makundi yaliyojihami nchini humo.

Mathalani makumi ya  watu waliofungwa jela kwa uhalifu wa kutowesha watu, kuua kwa halaiki, ukatili wa kingono na unyanyasaji wataachiwa huru katika kipindi cha saa 24.

Bi. Bachelet, kupitia taarifa  iliyotolewa leo mjini Geneva, Uswisi, amesema hatua hiyo huenda ikaathiri vibaya na kurudisha nyuma usimamizi wa sheria na uwajibishwaji ya mwaka 1996 kufuatia makubaliano ya amani yaliyomaliza miaka 36 ya mzozo.

Kamishna mkuu huyo amesema halikadhalika, uchunguzi dhidi ya ukatili utasitishwa, akionya kuwa hatua kama hiyo huenda ikahatarisha na kutonesha vidonda vya manusura na kuvunja imani na mamlaka na taasisi.

Kabla ya kupitishwa, muswada unahitajika kusomwa mara tatu ndani ya bunge ambapo tayari muswada ulisomwa Januari 17 mwaka huu kinyume na pendekezo la kamisheni ya haki za binadamu ya Guatemala