Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres asikitishwa na mlipuko wa bomba Mexico, aelezea mshikamano na mamlaka

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres
UN Photo/Mark Garten)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres

Guterres asikitishwa na mlipuko wa bomba Mexico, aelezea mshikamano na mamlaka

Amani na Usalama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameelezea kusikitishwa kwake na mlipuko kwenye bomba la mafuta katika jimbo la Hidalgo nchini Mexico jana, Januari 18 mwaka huu.

Kupitia taarifa ya msemaji wake, Bwana Guterres ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya wale waliopoteza wapendwa wao katika tukio hilo na kuwatakia ahueni ya haraka majeruhi.

Katibu mkuu huyo ameelezea mshikamano wake na watu na serikali ya Mexico.
Halikadhalika Umoja wa Mataifa umeelezea utayari wake kutoa msaada kwa mamlaka ya kitaifa.