Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunafuatilia hali ya DRC kwa karibu- OHCHR

Wapiga kura wakiangalia majina yao kwenye orodha ya wapiga kura wakati wa uchaguzi wa rais na wabunge huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC tarehe 30 Desemba 2018
MONUSCO/Alain Likota
Wapiga kura wakiangalia majina yao kwenye orodha ya wapiga kura wakati wa uchaguzi wa rais na wabunge huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC tarehe 30 Desemba 2018

Tunafuatilia hali ya DRC kwa karibu- OHCHR

Amani na Usalama

Tumekuwa tukifuatilia kwa karibu hali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, na tunaelewa kuwa mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi kesho tarehe 19 mwezi huu wa Januari.

Hiyo ni kauli ya msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa, OHCHR,  mjini Geneva Uswisi, Ravina Shamdasani wakatiakizungumza na waandishi wa habari akiongeza kuwa, “kwa mara nyingine, kile ambacho tumesema ni kwamba tunaomba utulivu pale matokeo yanapotangazwa”.

Bi. Shamdasani ameongeza kuwa kumeshuhudiwa uhasama na vurugu na kwamba, “nimepokea ripoti kutoka kwa wafanyakazi wenzangu asubuhi ya leo wakisema kuwa tangu kutangzwa kwa matokeo ya awali ya uchaguzi Ofisi ya haki za binadamu nchini humo imerekodi vifo 34,majeruhi 59 na watu 241 wamekamatwa nchini DRC”.

Kwa mantiki hiyo ofisi ya haki za bindamu imesema inasikitishwa sana na hali ilivyo sasa na imetoa wito kwa pande husika kutafuta mbinu za kusuluhisha uhasama kwa mazungumzo na sio kwa njia ya ukatili.

Matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika nchini humo tarehe 30 mwezi uliopita yalitangazwa Januari 9 mwaka 2019 ambapo Felix Tshisekedi alitangazwa kuwa  mshindi wa uchagui kwa kura asimilia 38.57 ya kura zote zilipigwa, na matokeo hayo yanasubiri kuthibitishwa rasmi na mahakama ya kikatiba.

 TAGS: DRC, Uchaguzi, Felix Tshisekedi, OHCHR