Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Faida ya teknolojia ya satelaiti katika ufugaji huko Mali.

Mitambo kama hii ya satelaiti, imesaidia katika kufanikisha maisha bora kwa watu duniani.
UN
Mitambo kama hii ya satelaiti, imesaidia katika kufanikisha maisha bora kwa watu duniani.

Faida ya teknolojia ya satelaiti katika ufugaji huko Mali.

Ukuaji wa Kiuchumi

Makala iliyochapishwa kwenye wavuti wa shirika la mazingira duniani,  UNEP inasema kuwa wafugaji wengi kwenye eneo hilo akiwemo Adoum ni wale wanaohamahama na mabadiliko ya tabianchi kwenye eneo hilo la ukanda wa Sahel yamesababisha ukame, maeneo yenye maji ni haba wakati wa msimu wa kiangazi na wanyama wengi wako katika hatari ya kufa kabla ya kufikia katika eneo la maji.

Abdoul Aziz Ag Alwaly ambaye ni mkuu wa programu ya shirika lisilo la kiserikali la TASSAGHT ambalo linashirikiana na wafugaji katika eneo la Sahel na pia ni mwanachama mwanzilishi wa mtandao wa wafugaji Afrika anasema “kabla ya kuamua pahali pa kupeleka mifugo, wafugaji walilazimika kuwalipa watu fedha ili waende kukagua eneo iwapo wanadhani kunaweza kuwa na maji na kisha watu hao hurudi kuleta taarifa ya walichokiona. Inaweza kuchukua siku kadhaa kupata taarifa kwa mwendo wa pikipiki n ahata wiki nzima ikiwa usafiri utakaotumika ni ngamia. Ni gharama, inachukua muda mrefu na ni hatari”

Hata hivyo UNEP inasema kupitia huduma ya simu ya Garbal wafugaji wanaweza kupokea kwenye simu zao za kiganjani picha za satelaiti, taarifa za maji na mahali kunakoweza kupatikana malisho ya mifugo yao na hivyo kuwaokolea muda, fedha na maisha ya mifugo yao.

Garbal ni huduma ya mtandao wa simu unaoendeshwa na kampuni ya simu ya Orange nchini Mali na huduma hiyo ilianzishwa  na wakulima kupitia mradi wao wa  STAMP ulioanzishwa mwaka 2017 ambapo ili kuitumia huduma hiyo, mtumiaji analazimika kujiunga na mtandao huo kwa malipo kidogo.

Adoum ni miongoni mwa wafugaji 21,000 walionufaika na huduma hiyo ya simu ya Garbal ya kutafuta maeneo mazuri ambako wanaweza kuielekeza mifugo yao.