Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Majengo na malighafi za ujenzi huchafua mazingira- UNEP

Majengo ambayo hayajakamilika mjini Cairo Misri.
World Bank/Kim Eun Yeul
Majengo ambayo hayajakamilika mjini Cairo Misri.

Majengo na malighafi za ujenzi huchafua mazingira- UNEP

Tabianchi na mazingira

Majengo na shughuli za ujenzi huchangia asilimia 39 ya hewa chafuzi ya ukaa, amesema  Marino Otto, mkuu wa kitengo cha miji kwenye shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira duniani, UNEP.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, Bi. Otto amesema kiwango hicho kinajumuisha hewa chafuzi zitokazo kwenye majengo mathalani kupitia hewa itolewa nje na viyoyozi pamoja na malighafi zitumikazo kujenga majengo hayo akisema kuwa majengo yaliyojengwa kwa saruji na vyuma  huchangia asilimia 11 ya uchafuzi wa mazingira.

“Viwanda vya saruji vinatarajiwa kuzalisha hewa chafuzi ya ukaa asilimia 5 ambayo itachochea kwa kiasi kikubwa katika mabadiliko ya tabianchi kama sekta moja. Sekta hiyo kwa kugundua changamoto hiyo inajizatiti kupunguza uchafuzi, lakini hiyo bado haitoshi.”

Bi. Otto amesema mbadala wa ujenzi ambao unajali mazingira ni ule unaotumia mbao ambazo amesema

“Tani moja ya saruji inatoa tani moja ya hewa ya ukaa wakati ikitengenezwa, na tani moja ya mbao kupitia miti ambako inatolewa inasaidia kuondoa tani 2 za hewa ya ukaa kutoka kwa mazingira.”

Ameongeza kuwa ni muhimu kuwa na usimamizi endelevu wa  misitu kwa kuhakikisha kuwa kila mti unaokatwa mwingine unapandwa ili kuzingatia ulinzi na  uhifadhi wa mazingira katika nyanja tofauti.