Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MINUSMA yafadhili redio za kijamii Mali

Radio ni mkombozi kwa watu wengi kwa kuwa  huwezesha kupata habari kwa kina kama hapa inavyoonekana kwa wakazi wa Sangari Jamhuri ya Afrika ya kati wakisikiliza Radio Lego Tila Ouaka( Sauti ya Ouaka) radio ya jamii inawaleta pamoja waislamu na wakristo
Picha ya OCHA/Gemma Cortes
Radio ni mkombozi kwa watu wengi kwa kuwa huwezesha kupata habari kwa kina kama hapa inavyoonekana kwa wakazi wa Sangari Jamhuri ya Afrika ya kati wakisikiliza Radio Lego Tila Ouaka( Sauti ya Ouaka) radio ya jamii inawaleta pamoja waislamu na wakristo

MINUSMA yafadhili redio za kijamii Mali

Amani na Usalama

Nchini Mali mradi uliofadhiliwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuongeza umbali wa masafa ya redio za kijamii umekuwa na mafanikio makubwa hasa kwenye maeneo yaliyo ndani zaidi na yenye miundombinu duni. 

Mjini Mopti katikati mwa Mali, nchi ambayo asilimia 33 ya wananchi wake hawajui kusoma na kuandika huku usalama ikiwa ni changamoto kila uchao.

Harakati za radio za kijamii kutumia matangazo yake ili kukwamua wananchi na kujenga  utangamano zilikumbwa na kikwazo baada ya matangazo kushindwa kufika umbali mrefu.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Mali, MINUSMA kwa kutambua umuhimu wa radio za jamii katika kusongesha amani na maendeleo ilitumia mradi wake wa matokeo ya haraka, QIP, kusaidia kuongeza mawanda ya usikivu wa radio hizo mjini Mopti.

Moja ya radio wanufaika ni Jamana ambayo Oumar Diabaté ni mkurugenzi wake.

“Wakati MINUSMA ilipokuja kutusaidia, mawanda ya redio hayakuzidi kilomita 60. Tangu tumepokea antena za kurahisisha urushaji matangazo wetu, imetusaidia kuwafikia wasikilizaji wetu wa zamani”

Bah Samake, muuza duka katika soko la Mopti ni msikilizaji wa mara kwa mara wa redio na anafunguka..

“Redio inabadili maisha yetu. Inatufanya tujihisi sehemu ya jamii. Tunaweza kufahamu tarehe na kinachotokea hapa. Tunapata habari za ukanda, tunapata habari za hapa nyumbani, tunasikia ujumbe”

Wakiwa wameathiriwa na mgogoro unaoendelea, watu wa Mopti, wanahitaji taarifa ambazo zimezingatia pande zote na kutolewa kwa wakati muafaka na kuna matumaini makubwa kuwa redio hizi tisa ambazo zimeongezewa nguvu na MINUSMA zimeanza kuliziba pengo.