Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guatemala hakikisha haki za msingi na uhuru taasisi- Bachelet

Askari akiwa katika doria katika jiji la Guatemala nchini Guatemala
World Bank/Jesus Alfonso
Askari akiwa katika doria katika jiji la Guatemala nchini Guatemala

Guatemala hakikisha haki za msingi na uhuru taasisi- Bachelet

Haki za binadamu

Kuelekea maandamano yanayotarajiwa kufanyika leo na kesho katika miji mbalimbali nchini Guatemala, kamishna mkuu wa haki za bindamu wa Umoja wa Mataifa, Michelle Bachelet amesihi  serikali ya Guatemala ihakikishe uhuru wa kujieleza na haki ya kuandamana kwa amani vinazingatiwa.

Bi Bachelet kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye wavuti wa Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa amesema, “uhuru wa kuijieleza, bila hofu ya kulipiza kisasi au kutishiwa ni uti wa demokrasia.” Ameongeza kuwa utamaduni wa haki za binadamu na amani unaimarika pale makundi yenye mitizamo tofauti inaweza kujieleza kwenye umma na kufurahia haki zao kwa uhuru.

Maandamano hayo yamepangwa na vyama mbalimbali vya umma kwa ajili ya kupinga mambo kadhaa ikiwemo maamuzi ya serikali kufuta mkataba wake na Umoja wa Mataifa kuhusu kamisheni ya kimataifa dhidi ya ukwepaji sheria nchini Guatemala CICIG.

Halikadhalika kamishna mkuu huyo ameelezea wasiwasi wake kuhusu kukandamizwa kwa taasisi nyingine za taifa ikiwemo uhuru wa mahakama, akiongeza kuwa taasisi hizo na maafisa wake wana mchango mkubwa katika kuheshimu na kuhakikisha haki za binadamu, sheria na demokrasia.

Bi. Bachelet ameongeza kuwa, utendaji wa kazi zake ni muhimu katika muktadha wa sasa na ili uchaguzi mkuu ufanyike katika miezi michache ijayo. “Kuheshimu usalama wao na familia zao ni lazima uhakikishiwe na mamlaka za Guatemala kwa mujibu wa kuzingatia sheria ya kimatifa ya haki za binadamu,”  amesema Bi Bachelet.

Aidha ameongeza kuwa yeye na ofisi yake nchini Guatemala wako tayari kushirikiana na mamalaka katika kuhakikisha wanatimiza ahadi na matarajio yake kuhusu haki za kimataifa.