Mafuriko na baridi kali vimesababisha shule kufungwa- Lebanon

14 Januari 2019

Theluji kali na upepo uliokumba kambi za wakimbizi wa Syria  nchini Lebanon sasa vimesababisha shule kufungwa huku Umoja wa Mataifa ukihaha kuwapatia wakimbizi mahitaji muhimu ya kukabiliana na hali ya baridi kali. 

Ni katika kambi ya Machareeh Al Qaa nchini Lebanon ambayo inahifadhi wakimbizi wa Syria ambako baridi kali imesababishaa mahitaji kuongezeka na hivyo Shirikla la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linasambaza vifaa vya kukabiliana na baridi kali.

Kupitia video ya Umoja wa Mataifa wakimbizi wanaonekana wamepanga foleni wakisubiri mgao kutoka kwa UNICEF.

Makazi ya muda ambako wakimbizi wanaishi yaliathiriwa na mvua kali ambako takriban watu 11,300 wameathirika, nusu yao wakiwa ni watoto.

Baada ya kupokea mgao huo, ni tabasamu huku watoto wakicheza nje kwenye mvua.

Mafuriko yamegubika makazi yao na watoto ambao sasa hawaendi shule wanalazimika kutumia mifagio ambalo kusukuma maji na wapate pahala pa kucheza.

Hali ikiwa hivi, UNICEF nayo inajiandaa kukabiliana na kimbunga kingine kinachotarajiwa kupiga Lebanon katika siku chache zijazo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter