Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu wakimbia mapigano kaskazini mashariki mwa Syria- UNHCR

Familia 400 zimepata hifadhi katika kituo cha makazi ya muda huko Idlib nchini Syria na watoto nao wamepata fursa ya kusomea kwenye mahema
© UNICEF/Aaref Watad
Familia 400 zimepata hifadhi katika kituo cha makazi ya muda huko Idlib nchini Syria na watoto nao wamepata fursa ya kusomea kwenye mahema

Maelfu wakimbia mapigano kaskazini mashariki mwa Syria- UNHCR

Wahamiaji na Wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeelezea kusikitishwa kwake na na ripoti za majeruhi wakiwemo wanawake na watoto na kufurushwa kwa idadi kubwa ya watu kufuatia mapigano mapya katika jimbo la  Deir-ez-Zor mashariki mwa Syria.

Akizungumza na waandishi wa habari mjni Geneva, Uswisi msemaji wa UNHCR, Andrej Mahecic amesema katika kipindi cha miezi sita, mapigano , mashambulizi ya anga kusini mashariki mwa jimbo hilo vimesababisha watu 25,000 kukimbia.

Ameongeza kuwa wanawake na watoto na wazee wako hatarini na kwamba,

“Inakadiriwa kuwa watu elfu mbili wako katika maeneo Hajin yaliyoathiriwa na mzozo . Wanaokimbia wanaelezea hali mbaya, huku huduma na bei za juu za chakula, tuna wasiwasi kuhusu watu walioko katika maeneo yanayoshikiliwa na wapiganaji wa ISIS.”

UNHCR inatoa wito kwa pande zote, na wale walio na ushawishi kuhakikisha uhuru wa kutembea na kuwafikia.

Halikadhalika, UNHCR katika taarifa yake imerejelea wito wake wa kuhakikisha uwasilishaji wa misaada hususan wakati huu wa msimu wa baridi kali.