Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MICT yashukuru Tanzania kwa mafanikio iliyoyapata

Rais wa taasisi ya kimataifa inayoshughulikia masuala yaliyosalia ya makosa ya jinai,MICT jaji Theodor Meron(kati kati) jaji William Sekule kulia kwake na Alvaro Rodriguez mwakilishi mkai wa UN Tanzania
UNIC Dar es salaam
Rais wa taasisi ya kimataifa inayoshughulikia masuala yaliyosalia ya makosa ya jinai,MICT jaji Theodor Meron(kati kati) jaji William Sekule kulia kwake na Alvaro Rodriguez mwakilishi mkai wa UN Tanzania

MICT yashukuru Tanzania kwa mafanikio iliyoyapata

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Rais wa taasisi ya kimataifa inayoshughulikia masuala yaliyosalia ya makosa ya jinai,MICT  jaji Theodor Meron leo ameshukuru serikali ya Tanzania kwa msaada wake kwa taasisi hiyo wakati akitoa hotuba yake kwenye Kongamano la Umoja wa Mataifa jijini Dar es Salaam.

Jaji Meron ametoa kwa serikali akisema bila msaada wa serikali hawangefika walipofika sasa akitaja kipande cha ardhi walichopewa katika eneo la Laki Laki vitongoji mwa Arusha, Tanzania Kaskazini ambapo wameweza kujenga mahakama na kumbukumbu zingine ikiwemo maktaba kuhusu sheria ya kimataifa kuhusu uhalifu.

Jaji huyo mkongwe amekaribisha wanafunzi na wanasheria kutumia hifadhi hizo ikiwemo maktaba akisema, “sisi wote ni washikadau na tunawaalika kutumia vifaa vyetu kama mpendavyo.”

Halikadhalika, Jaji Meron ameshukuru wafanyakazi wa taasisi hiyo akiwemo jaji William Sekule  kwa mafanikio yaliyopatikana.

Akizungumzia mafanikio ya taasisi hiyio, Jaji Sekule amesema..

(Sauti ya Jaji Sekule)

Jaji Sekule ametolea wito vijana kujihusisha na kile kinachowazunguka akisema kuwa ndio majaji wa kesho na hatimaye akatoa wito kwa wote akisema…

(Sauti ya Jaji Sekule)