Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN na AU zadhamiria kurejesha mazungumzo kati ya pande kinzani CAR

Maafisa polisi kutoka ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini  Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR wakiwa kwenye doria mjini Bouar nchini humo  katika picha hii ya Agosti 2018
MINUSCA/Hervé Serefio
Maafisa polisi kutoka ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR wakiwa kwenye doria mjini Bouar nchini humo katika picha hii ya Agosti 2018

UN na AU zadhamiria kurejesha mazungumzo kati ya pande kinzani CAR

Amani na Usalama

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix yupo ziarani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR kwa lengo za kuzindua tena mashauriano kati ya serikali na vikundi vilivyojihami. Assumpta Massoi na ripoti kamili.

Kwenye mji mkuu wa CAR, Bangui, Bwana Lacroix amewasili akiambatana na Kamishna wa amani na usalama wa Muungano wa Afrika, Smail Chergui na wanadiplomasia wengine.

Lengo ni kuzindua mazungumzo ya amani kati ya serikali na makindi yaliyojihami, mazungumzo yanayoratibiwa na AU ambapo amesema,

"Mwaka huu wa 2019 lazima uwe mwaka wa mabadiliko kwenye mazungumzo na maridhiano. Na tumedhamiris kufanya kazi pamoja kwa juhudi zote kufuata mwelekeo huo.”

Naye Bwana Cherguii ambaye kwa pamoja na Lacroix watakuwepo CAR kwa siku nne amesema,

"Jean-Pierre na mimi tumeamua hii kuwa hatua yetu ya kwanza kwa mwaka 2019 na kujikuta kwenye mji huu mkuu, tukiwa na mawaziri wa ukanda huu na wa CAR kujaribu kupatia chepuo utekelezaji wa mpango wa Afrika wa mazungumzo.”

Wakiwa nchini humo watakuwa na mazungumzo na viongozi mbalimbali akiwemo Rais Faustin-Archange Touadéra, Rais wa Bunge na wanasiasa.