Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 4,500 wamepoteza makazi Rakhine kutokana na mapigano kati ya serikali na Arakani Army

Mtoto akiwa katika makazi katika kambi ya Kyein Ni Pyin jimbo la Rakhine, Myanmar.
UNICEF/Ruslana Sirman
Mtoto akiwa katika makazi katika kambi ya Kyein Ni Pyin jimbo la Rakhine, Myanmar.

Watu 4,500 wamepoteza makazi Rakhine kutokana na mapigano kati ya serikali na Arakani Army

Amani na Usalama

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Mynmar Knut Ostby leo ameeleza kusikitishwa kwake na ripoti za vurugu katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar zilizotokea Januari 4 mwaka huu.

 

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric amewaambia wanahabri mjini New York kuwa, “Ostby, amesikitishwa na hali kule kaskazini na katikati mwa Rakhine ambako watu takribani 4,500 wamepoteza makazi hadi hivi sasa kutokana na mapigano kati ya kundi la Arakani Army (AA) na jeshi la Myanmar katika mwezi uliopita.

Dujarric amesema Umoja wa Mataifa umekuwa katika mawasiliano ya karibu na mamlaka za Myanmar katika wiki za hivi karibuni na wamekubali kuunga mkono juhudi za kusaidia walioathirika na vurugu hizo.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, serikali ya Myanmar imeanzisha operesheni dhidi ya inaowatambua kama waasi.Mapigano yaliendelea baada ya kundi la AA kufanya mashambulizi katika vituo vya polisi mjini Buthidaung. Watu walioyakimbia makazi yao wamejihifadhi  katika maeneo ya kijamii kwenye miji ya Kyauktaw, Ponnagyun, Rathedaung na Buthidaung. Mamlaka ya jimbo la Rakhine, msalaba mwekundu, mashirika ya kijamii na jamii wenyeji wamekuwa wakitoa uasaidizi hususani chakula na misaada mingine midogomidogo.