UNHCR yahakikishia Rahaf usalama wake wakati akisubiri jawabu ya ombi la uhifadhi

8 Januari 2019

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeelezea kutiwa moyo na hatua ya mamlaka Thailand kuruhusu Rahaf Mohammed Al-qunun kutoka kwenye hoteli ilioko kwenye  uwanja wa ndege, Bangkok na kwamba UNHCR iliruhusiwa kuonana naye na kwa sasa yupo maeneo salama mjini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi, msemaji wa UNHCR Babar Baloch amesema mchakato wa kutathmini maombi yake ya uhifadhi umeanza na

(Sauti ya Baloch)

“Tunatiwa moyo na mshikamano kutoka kwa watu kote ulimwenguni kuhusu ulinzi na usalama wake.”

Akijibu suali kutoka kwa mwaandishi wa habari kuhusu ripoti kuwa baba yake Rahaf anaelekea Bangkok, Baloch amesema

(Sauti ya Baloch)

"Siwezi kuthibitisha madai hayo, ila ningependa kurejelea kuwa usalama wake tuna wasiwasi nao, katika hatua hii ambapo amepitia changamoto hizo ni muhimu kwamba aondolewe katika mazingira hayo magumu, wafanyakazi wa UNHCR walikuwa naye jana, hofu yake ilikuw akwamba hataki kurudi katika hali ambapo Maisha yake yako hatarini na hivyo ni lazima tuheshimu matakwa yake kuhusu nani nanataka kuonana naye na asiyetaka kuonana naye.”

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo mbalimbali duniani, msichana huyu amekuwa akinyanyaswa na familia yake huko nchini Saudia Arabia na alifanikiwa kuikimbia familia hiyo wakiwa mapumzikoni nchini Kuwait.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud