Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zaidi zinahitajika kukabiliana na usafirishaji haramu kwenye mizozo-UNODC

Tokomeza usafirishaji wa binadamu. Kwa mujibu wa ripoti ya kimataifa ya UNODC asilimia 30 ya watu wanaosafirishwa kiharamu ni watoto.
UNODC
Tokomeza usafirishaji wa binadamu. Kwa mujibu wa ripoti ya kimataifa ya UNODC asilimia 30 ya watu wanaosafirishwa kiharamu ni watoto.

Hatua zaidi zinahitajika kukabiliana na usafirishaji haramu kwenye mizozo-UNODC

Haki za binadamu

Idadi ya waathirika wa usafirishaji haramu imeongezeka, huku idadi ya makundi yaliyojihami na magaidi wanawasafirisha wanawake na watoto kwa ajili ya kupata fedha na kuwaandikisha kama wafuasi, kwa mujibu wa ripoti ya takwimu za kimataifa kuhusu usafirishaji haramu wa watu iliyozinduliwa leo mjini Vienna, Austria.

Akiwasilisha ripoti hiyo ambayo imetathmini nchi 142 kuhusu mienendo ya usafirishaji haramu na uhalifu huo katika maeneo ya mizozo ya silaha, mkurugenzi mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupambamba na madawa ya kulevya na uhalifu, UNODC , Yury Fedeotov amesema, “watoto wanaotumikishwa jeshini, kazi ya lazima utumikishwaji kingono, usafirishwaji haramu umechukua sura mpya ya kusikitisha wakati vikundi vilivyojihami na magaidi wakisambaza hofu na kutumia vishawishi ili kuwapata wafuasi wapya.”

Bwana Fedotov amesema ripoti imeonesha wazi kuwa kuna haja ya kuimarisha ufadhili wa kiufundi na ushrikiano, kusaidia nchi kulinda manusura wake na kuwawajibisha wahalifu mbele ya sheria ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Akizunugmza katika hafla hiyo maalum ya kamisheni ya kuzuia uhalifu na uhalifu wa kisheria wakati wa uzinduzi huo waziri wa maswala ya kigeni wa Austria, Karin Kneissl, ametaja umuhimu wa ripoti kuangazia msaada kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na ukikwaji mkubwa wa haki za binadamu na utu.

Kimataifa, nchi zinagundua na kuripoti manusura wengi wa usafirishwahji haramu, kwa mujibu wa ripoti. Aidha ripoti imebaini kuwa kuna ongezeko la watoto wanaosafirishwa ikiwa ni asilimia 30 ya visa vyote huku wasichana wengi wakiathirika zaidi ikilinganishwa na wavulana. Ukatili wa kingono ndio kichocheo kikubwa cha usafirishaji haramu ikijumuisha asilimia 59 ya visa vyote.