Acheni mashambulio dhidi ya raia mjini Kabul: UNAMA

25 Disemba 2018

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA umelaani shambulio ambalo limetokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la mji mkuu Kabul na kusababisha vifo na majeruhi.

Katika taarifa iliyotolewa leo na UNAMA mjini Kabu, Afghanistan ujumbe huo unasema kuwa kwa sasa unajaribi kuthibitisha idadi ya watu waliouawa na majeruhi katika shambulio hilo ambalo limetokea katika ofisi za serikali. Miongoni mwa walioathirika ni wanawake.
Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, Tadamichi Yamamoto, amesema kuwa, “mashambulio haya yanasababisha mateso kwa binadamu na familia za wa Afghanistan.Umoja wa Mataifa unalaani vikali mashambulio hayo na hakuna sababu yoyote ya kuhalalisha mashambulizi ya aina hiyo.”

Hata hivyo amesema Umoja wa Mataifa unasisitiza kuwa wale wote ambao walipanga na kutekeleza mashambulio kama hayo ni lazima wachukuliwe hatua za kisheria na kuomba kwa mara nyingine tena pande zote husika kuheshimu wajibu wao chini ya sheria za kimataifa za kibinadamu wakati wowote ule ili kuwalinda raia wa kawaida dhidi ya mashambulizi.

Pia UNAMA imesema itaendelea kusimama kidete na watu wa Afghanistan na kuwa wamenuia kufuata mchakato wa amani ambao unaongozwa na watu Afghanstan wenyewe ambao utaweza kukomesha vita vinavyoendelea kwa hivi sasa nchini humo na kuiwezesha serikali kuweka raslimai za kuwalinda raia wote dhidi ya mateso kama hayo.

Bw. Yamamoto, kwa niaba ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan, ametuma salamu za rambirambirambi kwa familia za walioathirika na kuwatakia waliojeruhiwa ahueni ya haraka.

 

Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa, tafadhali jisajili na pia unaweza kupakua apu ili kuweza kusikiliza wakati wowote popote ulipo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud