Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pande zote husika Yemen heshimuni usitishwaji wa mapigano: Cammaert.

Generali Mraafu Patrick Cammaert, katika picha ya zamani.
UN Photo/Sophie Paris
Generali Mraafu Patrick Cammaert, katika picha ya zamani.

Pande zote husika Yemen heshimuni usitishwaji wa mapigano: Cammaert.

Amani na Usalama

Mafanikio au kushindwa kwa makubaliano ya mjini Stockholm, Sweden kati ya makundi husika na mgogoro wa Yemen yanategemea pande zote husika katika mgororo huo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa kamati ya uratibu wa mpangilio mpya huko Yemen -RCC- Jenerali Mstaafu Patrick Cammaert, akiwa mjinj Aden ambako aliwasili leo Jumamosi kwa ziara rasmi.


Katika taarifa iliyotolewa leo mjini New York Marekani na Stéphane Dujarric, msemaji wa Umoja wa Mataifa, Jenerali Cammaert, amekutana ana kwa ana na wajumbe wa serikali ya Yemen walioteuliwa kuwa katika kamati ya mpango wa RCC.


Katika mazungumzo hayo, Jenerali Cammaert, ameihimiza serikali ya Yemen pamoja na vikosi vya ushirika kudumisha usitishwaji wa mapigano ulioanza kutekelezwa usiku wa manane wa Desemba 18 na kuomba hakikisho lao pamoja na ushirikiano wa kuhakikisha misaada inaendelea kupita na kuwafikia walengwa nchi nzima.


Pia amezungumzia jinsi watakavyoweza kufanya mkutano wa kwanza wa RCC Hudaidah ama pembezoni mwake mapema 26.


Taarifa inasema kuwa Generali Cammaert anapanga kufunga safari hadi Sana’a hapo kesho ili kukutana na wajumbe walioteuliwa na wahouthi katika kamati ya RCC na pia kuwasilisha ujumbe kama huo kwao na baadae yeye na kundi lake wataelekea Hudaidah.

 

Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa, tafadhali jisajili na pia unaweza kupakua apu ili kuweza kusikiliza wakati wowote popote ulipo.