Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkataba wa Uhamiaji ukitekelezwa vizuri utalinda haki za wahamiaji.

Daktari mkimbizi kutoka Syria amtibu mgonjwa akiwa ukimbizini.
© UNHCR/Claire Thomas
Daktari mkimbizi kutoka Syria amtibu mgonjwa akiwa ukimbizini.

Mkataba wa Uhamiaji ukitekelezwa vizuri utalinda haki za wahamiaji.

Wahamiaji na Wakimbizi

Taarifa ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa iliyotolewa hii leo mjini Geneva Uswisi imesema watalaam hao wameupokea wito uliotolewa katika mkataba wa kimataifa wa uhamiaji salama, wenye mpangilio na unaofuata kanuni za kawaida ambao umepitishwa mjini Marrakesh,Morocco hivi karibuni.

Wito huo umezitaka nchi kushirikiana na sekta binafsi katika kulinda haki za wahamiaji na kuhakikisha wanagawana faida za kiuchumi wanazozalisha.

Dante Pesce, ambaye anaongoza kikundi cha wataalam wa Umoja wa Mataifa wanaojishughulisha na mambo ya biashara na haki za binadamu, Urmila Bhoola mtaalam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu aina mpya za utumwa na Felipe Gonzalez Morales mtaaalm huru wa Umoja wa Mataifa katika haki za binadamu za wahamaiaji kwa pamoja wamesema, “Kwa mara ya kwanza, nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Mataifa wanatambua kuwa njia ya kushirikiana ni muhimu kushughulikia faida za jumala za uhamiaji wakati wa kushughulikia hatari dhidi ya haki za binadamu na changamoto za mmoja mmoja na jumuiya katika nchi wanakotoka, wanakopita na wanakokwenda. Huu ni wakati muafaka”

Wataalam hao wamepongeza msisitizo wa mkataba katika ushirikiano wa taasisi za serikali na za binafsi na wakiongeza kuwa “Wahamiaji kote duniani mara nyingi wanakabiliwa na  mchakato mbaya wa jinsi wanavyopatiwa kazi, mazingira mabaya ya kazi, na kukosekana kwa usalama wao. Kimsingi changamoto hizi ni miongoni mwa changamoto kubwa ambazo jamii zetu zinakabiliana nazo” 

Wataalamu hao wamesema changamoto hizi zinazitaka serikali kuanza mara moja kutekeleza yale waliyokubaliana. Kwa mfano serikali zinaweza kuimarisha ukaguzi wa wafanyakazi ili kuhakikisha waajiri hawawanyang’anyi wahamiaji hati za kusafiria na nyaraka za utambulisho. Na kuwa pia serikali zinatakiwa kuongoza kwa vitendo katika taasisi za serikali na manunuzi ya umma.

Pia waajiri katika sekta binafsi wanatakiwa kuheshimu haki za wahamiaji na kuenesha mambo yao kwa namna ambayo itasaidi kutekeleza malengo ya mktaba wa Marrakesh kwa mfano kuhakikisha wahamiaji wanapewa mikataba iliyoandikwa na wanaelewa jinsi ya kuwasilisha malalamiko yao na kwa lugha wanayoielewa.