Uhamiaji uwe wa utu kwa kila mtu- IOM

18 Disemba 2018

Katika kuadhimisha siku ya uhamiaji duniani hii leo, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM, António Vitorino ametaka hatua zaidi na za dharura zichukuliwe ili kulinda kundi hilo ambalo kila uchwao linakumbwa na madhila kote ulimwenguni.

Kupitia ujumbe wake, Bwana Vitorino amesema pamoja na hatua hizo ni lazima utu upatiwe kipaumbele na ndio maana maudhui ya mwaka huu ya siku hii ya uhamiaji duniani wamechaguwa kuwa Uhamiaji na Utu.

Amesema kuhudumia wahamiaji wote kwa utu ni mahitaij ya kimsingi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile wakati huu ambapo mamilioni ya watu wanahama kwa hiari na wengine kwa lazima kutokana na sababu kama vile mabadiliko ya tabianchi na magonjwa kama vile Ebola huko barani Afrika.

Mkuu huyo wa IOM amesema pamoja na kusikiliza sauti za wahamiaji ni vyema pia kujibu hoja za shaka na shuku kwa wenyeji ambao wana wasiwasi juu ya ugeni, hivyo amesema..

(Sauti ya António Vitorino )

“Nikiwa Mkurugenzi Mkuu wa IOM, natoa wito kwa nchi wanachama na mashirika yakimaaifa waungane nasi kusherehehekea siku ya kimataifa ya uhamiaji tarehe 18 Desemba kwa kuchechemua uhamiaji salama, unaofuata kanuni na wenye utu kwa kila mtu.”

Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa, tafadhali jisajili na pia unaweza kupakua apu ili kuweza kusikiliza wakati wowote popote ulipo.

 

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter