Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukimbizi sio mwisho wa matumaini

Prise Josphine na Jemima Nsenga ni wakimbizi waliohamia nchi ya tatu Marekani, waliposhiriki hafla ya kukaribisha kupitishwa kwa mkata wa wakimbizi kwenye Umoja wa Mataifa.
UN News/Grece Kaneiya
Prise Josphine na Jemima Nsenga ni wakimbizi waliohamia nchi ya tatu Marekani, waliposhiriki hafla ya kukaribisha kupitishwa kwa mkata wa wakimbizi kwenye Umoja wa Mataifa.

Ukimbizi sio mwisho wa matumaini

Wahamiaji na Wakimbizi

Kuishi ukimbizini kuna changamoto kubwa lakini la msingi ni kukumbatia hali na kutia bidii kwa kila fursa uipatayo. Wito huo umetolewa na wasichana wawili wakimbizi ambao sasa wanaishi hapa Marekani baada ya kunufaika na mpango wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi , UNHCR wa kuwahamishia wakimbizi katika taifa la tatu. Wasichana hawa kabla ya kuja Marekani Prise Josephine mwenye umri wa miaka 16 raia wa Sudan aliishi kambini Kakuma Kenya kwa miaka 9 na Jemima Nsenga mwenye umri wa miaka 18  aliishi Uchina kama mkimbizi kwa miaka mitatu wamezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii