Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAHAMU: Mkataba wa kimataifa wa wakimbizi na mkataba wa kimataifa wa uhamiaji salama

Wafanyakazi wahamiaji wakiwa kazini katika kiwanda cha matofali huko Mawlamyine, Myanmar.
IOM
Wafanyakazi wahamiaji wakiwa kazini katika kiwanda cha matofali huko Mawlamyine, Myanmar.

FAHAMU: Mkataba wa kimataifa wa wakimbizi na mkataba wa kimataifa wa uhamiaji salama

Wahamiaji na Wakimbizi

Mkataba wa kimataifa wa wakimbizi: Tofauti ni ipi na mkataba wa wahamiaji na ni kwa vipi utasaidia watu waliolazimika kukimbia makwao?

Makubaliano mapya ya kuwezesha kushughulikia wakimbizi kwa njia thabiti na sawa yenye jina Mkataba wa Kimataifa kuhusu wakimbizi unatarajiwa kupitishwa na wanachama wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Jumatatu, kwa ajili ya kusaidia kwa kiasi kikubwa wale wanaokimbia makwao na nchi zinaziwahifadhi, ambazo mara nyingi ni zile maskini zaidi duniani.

Umeundwa kuwezesha mfumo mzuri na wenye mpangilio ili kuimarisha maisha ya wakimbizi na jamii zinazowahifadhi kufuatia miaka miwili ya majadiliano ya kina- ambayo yanafahamika kwa mtu yeyote ambaye amekuwa akifuatilia mwelekeo wa Mkataba wa kimataifa wa  Uhamiaji salama, wenye mpangilio na ulio wa kawaida uliopitishwa Marrakech nchini Morocco Jumatatu iliyopita.

Watoto wakiwa ndani ya darasa la shule ya hema ya UNICEF katika kambi ya Alhabanya,Anbar, Iraq.Watoto wahamiaji na wakimbizi hukosa elimu wanakokimbilia.
UNICEF/UN0161150/Anmar
Watoto wakiwa ndani ya darasa la shule ya hema ya UNICEF katika kambi ya Alhabanya,Anbar, Iraq.Watoto wahamiaji na wakimbizi hukosa elimu wanakokimbilia.

Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa imeandaa muongozo wa kutofautisha mhamiaji na mkimbizi na tofauti kati ya makubaliano hayo yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ambayo yanalenga kuimarisha maisha ya kila mtu anayehama.

Tumesikia kwamba mkataba wa uhamiaji umepitishwa hivi majuzi. Ni kwa nini tunahitaji mkataba mwingine?

Tamko la New York ambalo lilipitishwa Septemba 2016 liliibua mikataba miwili: mmoja kuhusu wakimbizi na mwingine ukilenga wahamiaji. Licha ya kwamba wote ni makundi ya watu ambao wanaishi nje ya nchi walikotokea, kuna tofauti muhimu kati ya “mkimbizi” na “mhamiaji”

Ni nini tofauti kati ya “mkimbizi” na “mhamiaji”? 

Wakimbizi: Ni watu ambao wako nje ya nchi yao ya kuzaliwa kwa sababu za kuogopa kunyanyaswa, mizozo, ukatili wa aina yoyote, au mazingira ambayo yanaweza kuathiri usalama wa umma na matokeo yake kusababisha ulinzi wa kimataifa. Maelezo ya mkimbizi yanaweza kupatikana katika mkataba wa 1951 na nyaraka zingine za kikanda kuhusu wakimbizi ikiwemo tamko la UNHCR .

Asilimia 20 ya taka za kielektroniki ndio hurejelezwa katika mazingira rasmi
Photo: UNICEF/Joshua Estey
Asilimia 20 ya taka za kielektroniki ndio hurejelezwa katika mazingira rasmi

Licha ya kwamba hakuna maelezo ya kisheria kuhusu mhamiaji wa kimataifa, wataalam wengi wanakubaliana kuwa mhamiaji wa kimataifa ni mtu ambaye anabadilisha makazi yake tofauti na kule alikozaliwa, bila kujali sababu ya yeye kuhama au uhalali wake uhamishoni. Kwa ujumla, kuna tofauti kati ya uhamiaji wa muda mfupi au uhamiaji wa muda, ukilenga uhamiaji unaodumu kati ya miezi mitatu hadi mwaka, na uhamiaji wa muda mrefu au wa kudumu, ukimaanisha kubadili nchi mtu anakoishi kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja au zaidi.

“Mimi’ni mhamiaji lakini sikuhitajika kuhatarisha maisha yangu katika boti iliyokuwa ikivuja maji au kulipa wasafirishaji haramu. Uhamiaji salama hauwezi kuwepo tu kwa wasomi au tabaka la juu ulimwenguni”, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.  

Je hii inamaanisha kuwa mkataba wa wakimbizi haufai kutumika?

Mkataba unajengea, na sio kuchukua nafasi ya mfumo ya kisheria uliopo kwa ajili ya wakimbizi ukiwemo mkataba wa 1951 kuhusu wakimbizi na mifumo mingine juu ya wakimbizi, haki za binadamu na sheria za kibinadamu.

 “Mkataba wa wakimbizi unalenga haki za wakimbizi na wajibu wa wa mataifa lakini hauzingatii ushirikiano wa kimataifa kwa kwa ujumla. Na hilo ndilo jambo ambalo mkataba wa kimataifa kuhusu wakimbizi unalenga kutatua”, alielezea Naibu Kamishna Mkuu wa UNHCR, Volker Türk. 
Mkataba wa mwaka 1951 hauweki bayana ni vipi nchi zitagawana mzigo na majukumu, lakini hicho ndicho Mkataba wa kimataifa unalenga. “Unatoa muongozo wa moja ya pengo kubwa ambalo tumekabiliwa nalo kwa miongo.”
Lakini ni kwa nini tunahitaji makubaliano mapya ya kimataifa?

Kufikia mwisho wa mwaka 2017, kulikuwa na wakimbizi takriban milioni 25.4 kote ulimwenguni, zaidi ya nusu wako chini ya umri wa miaka 18. Leo, nchi kumi zinahifahi asilimia 60 ya wakimbizi duniani. Uturuki pekee yake inawahifadhi wakimbizi 3.5 zaidi ya nchi nyingine yoyote. Zaidi ya hapo, wengi wa wakimbizi, yaani asilimia 85, wanaishi katika nchi zinazoendelea ambazo zinakabiliwa na changamoto zao za kiuchumi na kimaendeleo
Wafadhili kumi wa kiserikali (ukiwemo Muungano wa Ulaya) wanatoa takriban asilimia 80 ya ufadhili wa UNHCR, kwa mfano, na zaidi ya theluthi mbili ya maombi ya hifadhi ya UNHCR huenda katika nchi tano tu. Pengo kati ya mahitaji ya wakimbizi na hatua kukidhi mahitaji hayo ni kubwa na inaendelea kuongezeka.

Ni nani aliamua kubuni makataba huo? Ni UN au UNHCR?

Hapana, iliamuliwa na nchi wanachama. Azimio la New York kwa ajili ya wakimbizi na wahamiaji, lilipitishwa na nchi wanachama mwezi Septemba mwaka 2016 lilijumuisha hatua mbili muhimu kwa kuzingatia wakimbizi:
• Kwanza, cchi wanachama walipitisha muundo wa kina kuhusu namna ya kushughulikia wakimbizi au ‘CRRF’, ambao unaorodhesha taratibu za kufuata kukabiliana na mfumko mkubwa wa wakimbizi.
• Pili, nchi wanachama walikubaliana kuendelea kuimarisha mbinu za kimataifa za kukabiliana na wakimbizi kwa kufanya kazi kwa lengo la kupitisha mkataba wa kimataifa kuhusu wakimbizi mwaka  2018. Kwa mantiki hiyo waliwaomba Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR kujadiliana na nchi wanachama na wadau wengine na kupendekeza mkataba kama huo. Mkataba huo wa kimataifa kuhusu wakimbizi ulitolewa Julai 20, 2018.

Ni vipi mkataba kuhusu wakimbizi ulijadiliwa? 

Umebuniwa kutokana na utaratibu jumuishi na wa majadiliano na nchi wanachama na wadau wengine muhimu.
Mnamo mwezi Novemba 13, 2018, Kamati inayoangazia masuala ya kijamii, kibinadamu na kitamaduni ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ilipitisha azimio ambalo linaunga mkono mkataba wa wakimbizi kwa kura ya wengi na imetuma pendekezo hilo kwa Baraza Kuu kwa ajili ya kupitishwa rasmi, asubuhi ya Desemba 17, 2018.

Ni vipi mkataba wa kimataifa kuhusu wakimbizi utafanya kazi?

Mkataba wa kimataifa kuhusu wakimbizi unaweka msingi wa njia thabiti, inayotabirika na yenye usawa ya kukabiliana na idadi kubwa ya wakimbizi.
Licha ya kwamba haishurutishi kisheria, inatoa muongozo kwa jamii ya kimatifa katika kuwasaidia wakimbizi na nchi na jamii zinazowahifadhi wakimbizi wengi kwa kujenga azma ya kisaisa, na kupanua wigo wa msaada na kuweka mikakati ya kubeba mzigo wa wakimbizi kwa njia inayoeleweka na inayozingatia usawa/
“Wakimbizi ni jukumu la kimataifa na ni wajibu wa kila mmoja,” Kamishna Mkuu wa shirika la kuhudumia wakimbizi Filippo Grandi alisema. “Katika mkataba, kwa mara ya kwanza kutakuwa na mfano na mbinu zitakazowezesha kugeuza mkataba kuwa vitendo.”
 “Miongo ya kuwatenga wakimbizi, au katika kambi au kando na jamii kunaleta mbinu tofauti- ikiwemo wakimbizi katika mifumo ya kitaifa, jamii na chumi ya jamii zinazowahifadhi kwa muda unaohitajika na kuwawezesha kuchangia katika jamii wanakojso ma kujenga mustakabali wao, wakati wakisubiri kujua hatma yao. Grandi ameelezea, akitaja kuwa mkataba wa kimataifa ulianza na ukarimu wa jamii hizo.
 
Mkataba wa kimataifa una malengo manne:
1. Kupunguza mzigo kwa nchi zinazowahifadhi wakimbizi wengi;
2. Kuwawezesha wakimbizi kujitegemea; 
3. Kuwezesha wakimbizi kufikia nchi  ya tatu kupitia uhifadhi na njia zingine za kunigia nchini;
4. Kusaidia juhudi zinazowawezesha wakimbizi kurudi katika nchi walikotokea. 

Tayari nchi yangu inahifadhi wakimbizi wengi. Je tutasaidiwa?

Katika muktadha wa wakimbizi wengi, mkataba wa kimatifa unasema kuwa taifa au nchi walikotokea, inaweza kuomba UNHCR kuweka jukwaa la kusaidia katika utaratibu wa kushughulikia mfumo huo.
 “Kile tunataka kufikia ni kupata kwa haraka msaada: kisiasa, kifedha na kuwahifadhi, ili pale nchi zinakabiliwa na hali kama hiyo, wahisi kuwa hawako pekee yao, au wametengwa, au kwamba hamna anayewajali”, amesema Türk. “Kwamba jamii ya kimataifa inawajali watu, lakini nchi iliyoathirika. Na kwamba inasimama pamoja nao na inachukua hatua pamoja nao. Hayo ndio hasa”. 
Mkataba utakuwa na tofauti gani zinazoonekana kwa maisha ya wakimbizi na jamii zinazowahifadhi?

Naibu Kamishna Mkuu wa UNHCR alielezea kuwa iwapo mkataba utatekelezwa tutashuhudia “elimu bora kwa ajili ya wakimbizi wavulana na wasichana, pamoja na ufikiaji bora wa huduma za kiafya kwa wakimbizi wote na fursa nyingi za kimaisha”.  Jamii zinazowahifadhi wakimbizi zinaweza kuishi kwa njia tofauti na wakimbizi, na kuondokana na sera za kuwaweka kambini. 

Nchi zinazowahifadhi wakimbizi kwa mfano Uganda, Rwanda, Iran, na zile zilizoko Amerika ya Kati , au Lebanon- na miundombinu na huduma za kiafya zilizo na changamoto kwa kuhifadhi wakimbizi milioni moja- wanaweza kupata usaidizi wanaohitaji sio tu kwa mtazamo wa misaada ya kibinadamu lakini kutoka kwa mtazamo wa kushrikiana kimaendeleo. “Na hicho ndicho kipya”, ameongeza  Türk.  
Pia, UNHCR inalenga kupata maeneo zaidi ya kuhifadhi wakimbizi zaidi na kupata mbinu mpya ambapo wakimbizi wanaweza kuhamia nchi ya tatu, kwa mfano kuunganishwa na familia, udhamini wa wanafunzi, au visa za kimsaada.   

Lakini iwapo mkataba hauna masharti kisheria, utaleta mabadiliko?

Hauna masharti kisheria, lakini Umoja wa Mataifa utapitisha mkataba wa kimataifa. “Pindi tu hilo likifanyika, itaonesha azma kubwa ya kisiasa kwa nchi wanachama 193 kuitekeleza, licha ya kwamba haina masharti ya kisheria”, amesema Türk, akiongeza kuwa “katika Dunia ya leo hivyo ndivyo ushirikiano wa kimataifa unafanyika”.

Ni nani atafadhili hayo yote? 

Mkataba wa kimataifa unajumuisha majukumu kwa upana zaidi na kwa ushirikiano mkubwa zaidi. Inaangalia kile sekta binafsi, jamii za kidini na taasisi za kimataifa za fedha wanawaeza kuleta mezani.
Benki ya dunia imebuni mfumo mahsusi wa kifedha kwa nchi maskini zilizoathiriwa na ukimbizi- dola biloni 2 kwa miaka kadhaa, kuzisaidia kukabiliana na athari za kijamii na kiuchumi zinazotokana na wimbi la wakimbizi katika nchi. 

Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa, tafadhali jisajili na pia unaweza kupakua apu ili kuweza kusikiliza wakati wowote popote ulipo.