Biashara mtandaoni kiungo muhimu cha kufanikisha SDGs Afrika -UNCTAD

14 Disemba 2018

Afrika haitofikia malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs iwapo haitokumbatia fursa ya kuwekeza katika biashara ya mtandao, amesema Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi wakati wiki ya mkutano wa biashara mtandaoni barani Afrika ikifunga pazia leo Jijini Nairobi Kenya.

Akizungumza na Newton Kanhema wa Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa, mjini Nairobi kandoni mwa mkutano huo, Dkt. Kituyi amesema mkutano umeonesha wazi kuwa…

(Sauti ya Kituyi)

“Kuna watu wengi barani Afrika ambao wanaujuzi, nia na jitihada za kusongesha mbele SDGs kwa kutumia biashara mtandaoni kusongesha ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu. Wengi wamekubaliana hapa na wakaafikiana kuhusu mbinu za kuhamisha jumuiya ya mataifa ya Afrika, kuhamasisha wafanyakazi ,wawekezaji wa kiafrika kutumia hizi fursa kusaidia katika kukuza uchumi, kupunguza umaskini, kubuni ajira na kuendeleza mapato ya Afrika na kupanua wigo katika soko za biashara mtandaoni.”

Mkutano huo wa biashara mtandaoni ni wa kwanza kabisa kufanyika ukilenga  bara la Afrika, kwa lengo la kutoa taarifa na kuliweka bara hilokatika mazingira ambayo linaweza kufaidika na biashara mtandaoni.

Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa, tafadhali jisajili na pia unaweza kupakua apu ili kuweza kusikiliza wakati wowote popote ulipo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter