Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko magharibi mwa Niger yaacha watu 52,000 bila makazi.

Mama na mwana Niger.2018
UNFPA/Ollivier Girard
Mama na mwana Niger.2018

Machafuko magharibi mwa Niger yaacha watu 52,000 bila makazi.

Amani na Usalama

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema lina kutokana na ongezeko la machafuko katika maeneo ya mpaka wa Niger na nchi za Mali na Burkina Faso ambaye yamelazimisha   raia 52,000 wa Niger kukimbia makazi yao mwaka huu pekee.

Taarifa iliyotolewa leo na UNHCR inasema kuwa  mashambulizi ya mara kwa mara yanayofanywa na wanamgambo kwenye maeneo ya mpakani ya Niger ya Tillaberi na Tahoua,  yamesababisha watu wengi kusaka  maeneo salama kwenye miji na vijii vya karibu.

Raia wanaokimbia machafuko wanaeleza kuwa makundi ya watu waliojihami kwa silaha wanaripotiwa kushambulia vijiji, kuua na kuteka raia wa kawaida, wakiwemo viongozi wa jamii, huku wakichoma moto shule, na pia kupora mali kutoka nyumba za watu, biashara na pia mifugo.

Huku hali ya hatari iliyotangazwa na serikali ya Niger katika  maeneo ya mpaka ya Tahoua na Tillaberi  ikiendelea na kuwepo kwa idadi kubwa ya vikosi vya Sahel kutoka nchi tano au G5, bado hali ya kutokuwa na usalama pamoja na machafuko vinazidi kuzuia  juhudi za kutoa misaada ya kibinadamu.

UHNCR inasema kuwa tangu kuanza kwa mwezi Oktoba mwaka huu, , serikali ikishirikiana na  jamii zinazotoa misaada, imejaribu kupata maeneo salama ili kuhakikisha usambazaji  wa msaada, lakini tishio la usalama linazuia  wahusika kufikia maeneo yote ili kutoa msaada.

  Taarifa inaeongeza kuwa hali bado ni tete na mbali na kusababisha wimbi la wakimbizi wa ndani lakini pia machafuko hayo yamewaathiri wakimbizi wa Mali 53,000 waishio  maeneo ya Tillaberi na Thoua.

Baadhi wameiambia UNHCR kuwa wanatafakari kukimbilia maeneo ya kaskazini zaidi ama kwenda nchi zingine.

Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa, tafadhali jisajili na pia unaweza kupakua apu ili kuweza kusikiliza wakati wowote popote ulipo.