Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Biashara mtandaoni ikiwezeshwa yaweza kuliinua bara la Afrika :UNCTAD

 Katibu Mkuu wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii
UN News/Priscilla Lecomte
Katibu Mkuu wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii

Biashara mtandaoni ikiwezeshwa yaweza kuliinua bara la Afrika :UNCTAD

Ukuaji wa Kiuchumi

Mkutano wa biashara mtandaoni barani Afrika umefunguliwa rasmi leo mjini Nairobi Kenya kwa lengo la kuimarisha uwezo wa nchi za Afrika kushiriki na kunufaika na biashara mtandaoni na uchumi wa kidijitali.

Mkutano huo ulioratibiwa na Kamati ya Biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD umebeba kaulimbiu “Kuwezesha Uchumi wa nchi za Afrika katika zama za kidijitali.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo wa kwanza kabisa wa aina yake barani Afrika, Mkurugenzi Mtendaji wa UNCTAD, Dkt. Mukhisa Kituyi amesema kuwa sasa kuna ukuaji mkubwa wa biashara mtandaoni kote ulimwenguni na pia barani Afrika ikiwa ni asilimi 18 kwa mwaka lakini anahoji hali hii,“Huenda ni kweli kwamba watu milioni 21 wananunua huduma mtandaoni, huenda ni kweli kuwa watu milioni 134 wanatembelea mtandao wa Facebook lakini kweli kabisa kuwa hakuna kiwango cha maana cha huduma zinazouzwa kutoka Afrika mtandaoni, kwamba bidha kutoka Afrika zilizopo vijijini zinazouzwa na wanawake hazionekani popote katika soko ya kidijitali na hivyo tunahitaji mazungumzo ambapo walioweza wasaidie wengine.”

Ameongeza kuwa hawawezi kusherehekea kuwa Afrika imepiga hatua wakati asilimia 50 ya biashara mtandaoni inamilikiwa na Kenya, Afrika Kusini na Nigeria.Kwa upande wake rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, katika ufunguzi huo amesema ili Afrika iweze kupata faida za biashara mtandaoni...“Sera zinapaswa kuwa zinaweka mazingira rafiki na hivyo ni muhimu kwamba sekta hii ikapewa umuhimu unaohitajika.