Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asilimia 51 watu duniani watatumia intaneti ifikapo mwisho wa 2018-ITU

Watoto wanajifunza kompyuta sehemu za Chiang Rai Thailand. Vijana 12 walikwama  katika pango la eneo hilo na wameokolewa na kikosi maalum cha wapiga mbizi.
Picha: Tuenjai Chuabsamai/ESCAP
Watoto wanajifunza kompyuta sehemu za Chiang Rai Thailand. Vijana 12 walikwama katika pango la eneo hilo na wameokolewa na kikosi maalum cha wapiga mbizi.

Asilimia 51 watu duniani watatumia intaneti ifikapo mwisho wa 2018-ITU

Ukuaji wa Kiuchumi

Asilimia 51.2 ya watu wote duniani sawa na watu bilioni 3.9 watakuwa wanatumia mtandao wa intaneti ifikapo mwishoni mwa mwaka huu wa 2018, kwa mujibu wa makadirio mapya yaliyotolewa leo na ITU ambalo ni shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya habari na teknolojia ya mawasiliano au ICTs.

Akizungumzia makadirio hayo ya ripota ya upimaji wa teknolojia ya mawasiliano katika jamii katibu mkuu wa ITU Houlin Zhao amesema makadirio hayo ya ITU ya kimataifa na kikanda kwa 2018 ni ishara ya mafanikio makubwa yanayofanywa na dunia kuelekea kuwa na jumuiya jumuishi ya mawasiliano kimataifa.”

Ameongeza kuwa “Ifikapo mwisho wa 2018 tutapia kiwango cha 50/50 cha matumizi ya intaneti. Na hii ni hatua kubwa ya kuwa na jumuiya jumuishi ya mawasiliano, hata hivyo bado kuna watu wengi sana duniani wanasubiri kufaidi matunda ya uchumi wa kidijitali. Ni lazima tuchagizeuwekezaji zaidi kutoka sekta za umma na binafsi , kuweka mazingira mazuri ya kuvutia wawekezaji, na kuunga mkono teknolojia na biashara bunifu ili mapinduzi ya teknolojia yasimwache yeyote nje ya mtandao”

ITU inasema makadirio hayo yanaonyesha kwamba kunaendelea kuwa na mwenendo wa kuongezeka kwa fursa ya watu kupata na kutumia habari na mawasiliano ya teknolojia  pia fursa ya mitandao ya mawasiliano inaendelea kuongezeka hususan katika simu za kiganjani au za rununu. Licha ya mafanikio hayo ripoti inasema bado uwezo wa kumudu mawasiliano hayo ni mtihani ambao utaendelea kupewa kipaumbele na shirika hilo ili kuhakikisha uchumi wa kidijitali ni ndoto inayotimia kwa wote.

 Idadi ya watu wanaotumia intaneti

 Kwa mujibu wa ITU katika Mataifa yaliyoendelea ongezeko sio kubwa sana japo idadi inaendelea kupanda ya watu wanaotumia intaneti ikitoka asilimia 51.3 mwaka 2005 na kufikia asilimia 80.9 mwaka 2018. Na katika Mataifa yanayoendelea ongezeko limekuwa kubwa sana kutoka asilimia 7.7 mwaka 2005 hadi kufikia asilimia 45.3 mwisho wa mwaka 2018 huku ukuaji mkubwa ukiripotiwa barani Afrika  ambako asilimia ya watu wanaotumia inaneti imeongezeka kutoka asilimia 2.1 mwaka 2005 na kufikia asilimia 24.4 mwaka 2018.

Kwa mujibu wa ripota hii maeneo yaliyokuwa na ukuaji mdogo wa watumiaji wa intaneti ni Ulaya na Marekani  na kwa nchi za jumuiya ya Madola watu watakaokuwa wakitumia intaneti kufikia mwisho wa mwaka huu itakuwa ni zasilimia 71.3 , kwa matifa ya nchi za Kiarabu asilimia 54.7 wakati maitaifa ya Asia itakuwa asilimia 47.

Matumizi ya simu za rununu

Mtoto wa kimasai nchini akipata maarifa kupitia simu ya kiganjani .
Picha/Worldreader
Mtoto wa kimasai nchini akipata maarifa kupitia simu ya kiganjani .

Fursa ya matumizi ya simu za rununu kwa huduma ya kawaida ya mawasiliano inazidi kutawala, huku usajili wa matumizi ya simu za ndani ukizidi kupungua kutokana na ongezeko la asilimia 12.4 ya simu za runini kwa mwaka 2018, Na hivi sasa ITU inasema idadi ya usajili wa matumizi ya simu za rununu ni mkubwa kuliko idadi ya watu duniani.