Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kituo kipya cha UNHCR chaleta nuru kwa wakimbizi Libya

Nchini Libya wahamiaji hulalawakiwa wamebanana katika seliambazo zimejaa pomoni katika kituo chakuwazuilia cha Tariq al Sikka mjini Tripoli.
Photo: UNHCR/Iason Foounten
Nchini Libya wahamiaji hulalawakiwa wamebanana katika seliambazo zimejaa pomoni katika kituo chakuwazuilia cha Tariq al Sikka mjini Tripoli.

Kituo kipya cha UNHCR chaleta nuru kwa wakimbizi Libya

Amani na Usalama

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa ushirikiano na serikali ya Libya na washirika wa misaada, juma hili wamefungua kituo kipya cha wakimbizi mjini Tripoli, ili kuwapa wakimbizi hao mbadala salama badala ya kuwekwa kizuizini, wakati suluhu ya muda mrefu kama makazi ya kudumu na kuwasafirisha ikisawa. 

Mjini Tripoli katika kituo cha kwanza cha aina yake cha kuwakusanya na kuwasafirisha wakimbizi, GDF na kuwapatia mazingira salama wakisubiri hatma yao ya muda mrefu, ikiwa ni pamoja na kupewa makazi ya kudumu katika taifa lingine, kuunganishwa na familia zao, kuhamishwa kwenda kwenye vituo vya dharura katika nchi zingine, kurejeshwa kwenye nchi waliozopewa hifadhi awali n ahata kuwarejesha nyumbani kwa hiyari. Paula Barrachina Esteban ni msemaji wa UNHCR akiwa kwenye uwanja wa ndege wa Tripoli kuwahamisha baadhi ya wakimbizi wa kwanza waliokuwa kituoni hapo

“Wakimbizi hawa waliletwa kutoka katika vituo mbalimbali walikokuwa wanashikiliwa ili watumie siku zao za mwisho katika kituo hiki ambacho UNHCR inatoa mazingira bora kwa watoto, huduma ya afya kwa saa 24 siku saba kwa wiki, malazi bora na eneo salama na mbadala wa kizuizini.”

UNHCR inasema kukiwa na takriban wakimbizi na wahamiaji 5200 wanaozuiliwa kwenye vituo mbalimbali nchini Libya wakiwemo 3900 wanaohitaji ulinzi wa kimataifa, GDF ni mbadala muhimu sana cha kuwatoa kizuizini waltu walio katika hatari hususani wanawake , watoto na wagonjwa.

Kituo hiki ni mradi unaoendeshwa na wizara ya mambo ya ndani ya Libya, , UNHCR na mshirika mkubwa wa UNHCR, LibAid kwa msaada wa Muungano wa Ulaya na wahisani wengine kina wafanyakazi maalumu ambao wanahakikisha wakimbizi na waoomba hifadhi wanapatiwa huduma ipasavyo. Mradi huu ni moja ya hatua zinazohitajika ili kuwaepusha wakimbizi na wahamiaji kuchukua safari za hatari za boti kupitia bahari ya Mediterrania.