Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uuzaji wa bidhaa nje huenda ukaongezeka kwa asilimia 10.4 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu- UNCTAD

Biashara ya kimataifa inaongezeka Brazil
Santos Municipality
Biashara ya kimataifa inaongezeka Brazil

Uuzaji wa bidhaa nje huenda ukaongezeka kwa asilimia 10.4 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu- UNCTAD

Ukuaji wa Kiuchumi

Kiwango cha uuzaji wa bidhaa nje ya nchi huenda kikaongezeka kwa asilimia 10.4 mwaka huu na kufikia thamani ya dola trilioni 19.6, limesema chapisho la Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD.

Takwimu hizo ni kufuatia makadirio ya mwenendo wa sasa wa biashara ya bidhaa na huduma  zinazouzwa nje, ambayo inaendana na ukuaji ulioshuhudiwa mwaka 2017 ambapo biashara ya bidhaa iliongezeka kwa asilimia 10 baada ya miaka miwili ya kudorora na biashara ya huduma iliongezeka kwa asilimia 9.5.

Chapisho limetaja baadhi ya mambo ambayo yamechangia kukua kwa biashara hiyo mwaka 2017 na 2018 zikihusishwa na ukuaji wa pato la taifa kwa asilimi3.1 pamoja na ongezeko la bei ya bidhaa kwa asilimia 17,7 hususan mafuta kwa asilimia 26,1 na madini na vyuma kwa asilimia 12.2 kwa mujibu wa takwimu za UNCTAD.

Kwa mujibu wa UNCTAD, hali hiyo ni ishara ya kupungua kwa tofauti za ufanyaji biashara kati ya mataifa yaliyoendelea na yale yanayoendelea.

UNCTAD katika chapisho hilo imeangazia mambo matatu muhimu ikiwemo: ununuzi wa biashara kimataifa, biashara ya huduma kimataifa na pato la taifa, ikiwa ni hatua kufuatia kuongezeka kwa mahitaji ya taarifa kwa ajili ya kufuatilia biashara kimataifa, kuelewa athari za maendeleo kiuchumi au kisiasa na kuchangia katika utungaji sera.