Tanzania iimarishe hatua kuepuka mgongano wa maslahi kwenye utendaji- CAG
Mkutano wa wajumbe wa jopo la wakaguzi wa nje wa Umoja wa Mataifa ukimalizika leo kwenye makao makuu ya umoja huo jijini New York, Marekani, Tanzania ambayo ni mjumbe wa jopo hilo imesema imekuwa ni fursa ya kubadilishana mawazo hususan masuala ya kuepusha mgongano wa maslahi, udanganyifu na rushwa.
Katika mkutano huo, Tanzania inawakilisha na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali Profesa Mussa Assad ambaye katika mahojiano maalum na Arnold Kayanda wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, amesema wamejifunza mengi hususan taratibu za kuepusha mgongano wa maslahi
Tanzania imeteuliwa kuwa mtazamaji wa bodi ya ukaguzi ya Umoja wa Mataifa sambamba na mjumbe wa jopo la wakaguzi wa nje, na hii ni baada ya kuwa mjumbe wa bodi ya ukaguzi ya Umoja wa Mataifa kwa miaka sita, ujumbe ambao ulimalika mwezi Julai mwaka huu.