Kuna pengo la ujumuishwaji katika ulemavu na maendeleo:UN Ripoti

Binti wa miaka 15 kutoka tanzania, anasema upasuaji wa kurekebisha mdomo sungura umebadili maisha yake
CCBRT/Dieter telemans
Binti wa miaka 15 kutoka tanzania, anasema upasuaji wa kurekebisha mdomo sungura umebadili maisha yake

Kuna pengo la ujumuishwaji katika ulemavu na maendeleo:UN Ripoti

Haki za binadamu

Umoja wa Mataifa leo umezindua ripoti yake ya kwanza kabisa kuhusu ulemavu na maendeleo ambayo imetolewa na kuchapishwa na watu  wenye ulemavu kwa ajili ya kundi hilo, kwa matumaini ya kuchagiza fursa zaidi na kuwa na jamii jumuishi zisizowaacha nyuma watu wenye ulemavu.

Ripoti hiyo kuhusu ulemavu na maendeleo 2018imetolewa sanjari na maadhimisho ya siku ya walemavu duniani, ambayo kila mwaka huwa Disemba 3 ambayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameilelezea kama ni muhimu kwa ujumuishwaji wa kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa wote wakiwemo watu wenye ulemavu kama ilivyoainishwa kwenye malengo ya maendeleo endelevu au SDGs

Ripoti hiyo inaonyesha ni jinsi gani ubaguzi kwa misingi ya ulemavu ulivyo na athari katika mifumo ya usafiri, utamaduni na fursa za kushiriki katika maeneo ya umma na huduma. Na ripoti hiyo inatoa msukumo wa kufanya mabadiliko ya mazingira ya mijini na kuyanfanya yawe rahisi kujumuisha watu wenye ulemavu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo changamoto hizo mara nyingo hazionekani kwa sababu ya kutokuwepo kwa maswali ya kutosha kuhusu ulemavu, na athari zake kutokana na makadirio yasiyo sahihi ya idadi ya watu wanaoishi na ulemavu na kuathiriwa na ubaguzi na vikwazo vingine. Mwaka 2006 Umoja wa Mataifa ulipitisha mkataba kuhusu haki za watu wenye ulemavu na vipengele vyake kwa lengo la kulinda haki na utu wa watu wenye ulemavu , ambao unahitaji pande zote husika kuchagiza na kulinda haki za binadamu za watu hao.

Javier Vasquez, ambaye anasaidia kuongoza idaya ya afya ya  Olimpiki maalum kama mwkamu wa Rais  amesisitiza muingiliano uliopo baina ya haki za binadamu na afya linapokuja suala la watu wenye ulemavu.

“Wakati watu wenye ulemavu wanaweza kufurahia upatikanaji wa haki za binadamu, hili linadhihirika katika hali yao ya afya ya akili na mwili.”

Pia ameunga mkono suala la mapengo katika ujumuishwaji na uwakilishi na jinsi gani haya yanaweza kuathiri uelewa kuhusu watu wenye ulemavu na maisha yao.

Ameongeza kuwa kwa wastani watu wenye ulemavu kufariki duinia miaka 16 mapema Zaidi ya wasio na ulemavu, hata hivyo “Watu wengi hudhani kwamba watu wenye ulemavu hufariki dunia mapema kutokana na ulemavu wao nah ii sio kweli, tatizo ni kwamba maradhi haya kwa muktanda wa watu wenye ulemavu hayapimwi na hayagunduliki na matokeo yake yanaendelea kwa muda katika maisha yao bila kutibiwa. Mara nyingi watu hawa hawajumuishwi kwa sababu ya unyanyapaa na ubaguzi.”

Bwana. Vasquez ametoa wito wa kufanyika utafiti wa kina kuhusu changamoto na mafanikio ya watu wenye ulemavu kwa ajili ya kuunga mkono vuguvugu la kutaka fursa sawa katika haki za kisiasa, elimu na afya.Kwani amesema “Huwezi kukuta takwimu katika mifumo ya afya ya kitaifa hivyo tunashirikiana nanyi takwimu hizi ili kufanya watu hawa watambulike.”