Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maombi ya hakimiliki yazidi kuongezeka duniani- WIPO

Mkurugenzi Mkuu wa WIPO, Francis Gurry.
WIPO/Emmanuel Berrod
Mkurugenzi Mkuu wa WIPO, Francis Gurry.

Maombi ya hakimiliki yazidi kuongezeka duniani- WIPO

Ukuaji wa Kiuchumi

Ripoti mpya ya shirika la hakimiliki duniani, WIPO imeonyesha ongezeko la mahitaji ya hakimiliki am ambapo mwaka 2017 maombi yalivunja rekodi, China ikiongoza.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya viashiria vya hakimiliki iliyotolewa leo huko Geneva, Uswisi, kwa mara ya kwanza inajumuisha takwimu kuhusu uchumi bunifu, ikitokana na utafiti uliofanywa kwa pamoja na chama cha kimataifa cha wachapishaji ikihusisha mataifa 28.

“WIPO inasema ubunifu unaochochewa na hakimiliki umezidi kuwa kigezo cha ushindani na biashara ukizidi hata kasi ya ukuaji wa uchumi duniani,” ameseam Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Francis Gurry.

Ripoti inaonyesha kuwa bara la Asia limeongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya maombi ya hataza ambapo ofisi ya WIPO iliyoko barani humo ilipokea asilimia 65.1  ya maombi yote ikiwa ni ongezeko kutoka asilimia 49.7, miaka 10 iliyopita, ongezeko hilo likichochewa na ukuaji wa uchumi nchini China.

Bwana Gurry amesema “Asia hivi sasa imechangia theluthi mbili ya maombi yote ya hataza duniani na hii ni mabadiliko  ya aina yake ambayo yametokea katika kipindi kifupi.”

Kwa uchanganuzi maombi ya hakimiliki kutoka China kwa mwaka 2017 yaligusia hataza, nembo za biashara, ubunifu wa viwandani na hakimiliki nyingine na hivyo ikionyesha kuwa China ina idadi kubwa ya maombi kwa ajili ya wabunifu na wagunduzi.

Carsten Fink, ambaye ni mchumi mkuu wa WIPO amesema kuwa, “siyo China pekee, bali pia tunashuhudia ongezeko maradufu la maombi ya hakimiliki katika nchi nyingine kuanzia Marekani, Japan na pia kwa nchi ambazo zinaongoza kiuchumi mfano Ujerumani, Brazil, Canada, Uingereza. Brazil bila shaka, nchi ya  uchumi wa kati, na haya ni masoko yaliyokomaa, hivyo kuona aina hii ya ukuaji, nadhani ni jambo jema.”