Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Danai Gurira wa Black Panther ateuliwa kuwa balozi mwema wa UN Women

Mkurugenzi Mtendaji wa UN Women Phumzile Mlambo-Ngcuka akiwa na balozi mwema wa UN Women Danai Gurira, Johannesburg, Afrika Kusini.
UN Women
Mkurugenzi Mtendaji wa UN Women Phumzile Mlambo-Ngcuka akiwa na balozi mwema wa UN Women Danai Gurira, Johannesburg, Afrika Kusini.

Danai Gurira wa Black Panther ateuliwa kuwa balozi mwema wa UN Women

Wanawake

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake,UN Women, limemteua muigizaji maarufu wa filamu Danai Gurira kuwa balozi mwema ambaye atatumia jina lake na kujitolea kwake katika kushughulikia masuala ya usawa wa kijinsia na haki za wanawake ikiwa ni pamoja na kuzipa nafasi sauti za wanawake ambazo hazijasikika. 

Uteuzi huo umefanyika leo tarehe 2 desemba mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini wakati wa mkutano wa siku 16 za harakati dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Mkurugenzi Mtendaji wa UN Women Phumzile Mlambo-Ngcuka akizungumzia uteuzi huo amesema, “UN Women inayo furaha kumkaribisha Danai Gurira katika jukumu lake jipya la balozi mwema kuunga mkono kazi yetu ya usawa wa kijisia. Kama muigizaji na mwanaharakati wa usawa wa kijinsia, kwa kutumia lensi yake kali ya haki za binadamu, anafaa kipekee kuwasiliana na kuhamasisha. Anatambua changamoto na ataunganisha utofauti wa wanawake wanaoishi pembezoni mwa jamii. Ushirikiano wa Danai na sisi utaleta mstakabali bora kwa vizazi vingi vijavyo vya wasichana”.

Mcheza filamu na mwanaharakati Danai Gurira (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa UN Women Phumzile Mlambo-Ngucka, (katikati), pamoja na mcheza filamu na mwanaharakati Reese Witherspoon (kulia) wakati wa maadhimisho ya mwaka huu ya siku ya wanawake duniani.
UN Women Twitter

Gurira ni mmarekani wa kwanza mweusi mwenye asili ya Zimbabwe kuwa balozi mwema wa UN Women. Mashabiki zake humfahamu kama “General Okoye” kutokana na ushiriki wake wa hivi karibuni katika filamu maarufu ya Black Panther wengine wakiita Wakanda na ile ya Avengers: Infinity War.