Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa G20 wakamilika, UN yapokea azimio.

Katibu Mkuu wa  UN António Guterres akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa G20 huko Buenos Aires Argentina Novemba 29, 2018
UN News/Natalia Montagna
Katibu Mkuu wa UN António Guterres akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano wa G20 huko Buenos Aires Argentina Novemba 29, 2018

Mkutano wa G20 wakamilika, UN yapokea azimio.

Ukuaji wa Kiuchumi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amepokea tamko la mkutano wa nchi 20 zilizoendelea kiuchumi linaloelezea nguzo nne zilizopewa mkazo katika mkutano huo ikiwa ni mustakabali wa kazi, miundombinu ya maendeleo, maendeleo ya chakula endelevu na mkakati wa kuimarisha jinsia kwa kupima matokeo kwa watu wa jinsia tofauti ya sera zilizopangwa katika ajenda ya G20.

Mkutano huo umekamilika huko Buenos Aires, Argentina, nchi ambayo imejipambanua kujitolea kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

Kupitia katika taarifa iliyotolewa leo jumapili, Guterres amechagua maeneo matatu kutoka  tamko hilo la mkutano wa nchi zilizoendelea akianza na ajenda ya mwaka 2030.

Mosi ni kuunga mkono ajenda ya mwaka 2030 kwa maendeleo endelevu, mpango wa Umoja wa Mataifa wa utandawazi wa haki ambao haumwachi nyuma yeyote, umehakikishiwa katika waraka huo, pamoja na ahadi ya kutumia zana zote za sera ili kufikia ukuaji imara, endelevu, wenye uwiano na umoja.

Katika upande wa mabadiliko ya tabia nchi, Guterres amesema viongozi wa G20 wanasisitiza kuunga kwao nchi ambazo walitia saini mkataba wa Paris wa mwaka 2015, ili kutekeleza ahadi zao zilizowekwa katika michango yao ya kitaifa.

Na kuhusu ushirikiano wa kimataifa, Katibu Mkuu Guterres amesema viongozi wa G20 wanaelewa umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika biashara na marekebisho ya shirika la biashara duniani.