Ukitambua hali yako VVU si hukumu ya kifo- Muathirika

30 Novemba 2018

Je, wewe umepima afya yako kutambua iwapo una Virusi Vya Ukimwi, VVU au la? Nchini Tanzania mkazi mmoja alitambua hali yake na anaishi kwa matumaini kwa takribani miongo mitatu sasa!

Katika kuelekea siku ya ukimwi duniani ambayo kila mwaka huwa Disemba Mosi, wito umetolewa kwa watu kupima na kutambua hali zao, na kuishi kwa matumaini.

Wito huo ndio uliobeba kauli mbiu ya siku ya ukimwi mwaka huu .

Kujitokeza na kupima si kazi rahisi na hata wanaojitokeza na kufanya hivyo baada ya kutambua wameaathirika na virusi vya ukimwi au VVU na ni changamoto kuikubali hali na kuishi kwa mauamaini.

Hata hivyo kuna baadhi ya watu ambao wana ujasiri wa kutambua umuhimu wa kujua hali zao na kunusuru wengine dhidi ya janga la ukimwi ambalo kwa mujibu wa takwimu za shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi, UNAIDS mwaka 2017 kulikuwa na watu milioni 36.9 kote duniani wanaoishi na VVU, milioni 21.7 kati yao wakitumia dawa za kupunguza makali ya ukimwi na maambukizi mapya yalikuwa milioni 1.8.

Kutoka Radio washirika Huheso FM ya mjini Kahama mkoani Shinyanga nchini Tanzania Michael Francis Bundala amemtembelea William Martini mkazi wa Kahama anayeishi na VVU kwa takriban miongo 3.

(Mahojiano)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter