Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa kuboresha lishe wazinduliwa Uganda: UNICEF/WFP

Wanawake kwenye kituo cha afya, eneo la Karamoja. Picha ya UNICEF Uganda.

Mradi wa kuboresha lishe wazinduliwa Uganda: UNICEF/WFP

Afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la mpango wa chakula duniani , WFP leo wamezindua mradi wa kuboresha huduma za lishe miongoni mwa watoto katika eno la Karamoja Kaskazini Mashariki mwa Uganda Kwa msaada kutoka kwa Uingereza.

Uingereza imetoa Euro milioni 28 karibu swa na dola milioni 31.5 katika kuitikia tatizo la utapiamlo katika wilaya nane za eno la Karamoja. Mradi huu uliozinduliwa wilayani Kotido utatekelezwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa ya UNICEFT na WFP kwa kuhakikkisha kwmaba watoto na akinamama katika eneo hilo wanpata fursa ya kufikia huduma  stahiki za afya na lishe.

Dokta Doreen Mulenga ambaye ni  Mwakilishi wa UNICEF Uganda amesema msaada huu umekuja wakati muafaka ikizingatiwa kwamaba kila mtoto mmoja kati ya watatu anadumaa kutokana na lishe duni, hivyo mradi huu ni muhimu kwa afya zao.

Mama akiwa kando mwa mtoto wake alie lala akiwa na utapiamlo
UNICEF/UN055334/Tremeau
Mama akiwa kando mwa mtoto wake alie lala akiwa na utapiamlo

Ameongeza kuwa asilimia 84 ya watu wa Karamoja hawana uwezo wa  kupata milo yenye lishe kila siku, huku asilimia 45 ya watu binafsi hawawezi kupata chakula. Mradi huu unalenga watoto zaidi ya 100,000 walio chini ya Umri wa miaka mitano ambao wanakabiliwa na utapiamlo kupitia miradi ya lishe yua kijamii.

Utapiamlo ni changamoto kubwa katika mipango ya kuhakikisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika eno la Karamoja. Karibu watoto 15,000 wanokabiliwa na utapiamlo uliokithiri watapatiwa tiba maalumu hospitalini na kwenye vituo vya afya.

Mkurugenzi wa EFP, Uganda, El-Khidir Daloum amesema walikuwa wamestushwa na kiwango cha watoto wanaodumaa Karamoja ambacho kamwe hakiwezi kukubaliwa.