Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maabara mpya ya IAEA yazinduliwa kukabili changamoto za chakula na kilimo

Mtafiti akizipima nyanya katika maabara ya chakula na mazingira ya IAEA huko Seibersdorf, Austria.
IAEA
Mtafiti akizipima nyanya katika maabara ya chakula na mazingira ya IAEA huko Seibersdorf, Austria.

Maabara mpya ya IAEA yazinduliwa kukabili changamoto za chakula na kilimo

Ukuaji wa Kiuchumi

Shirika la kimataifa la nguvu za atomic , IAEA leo limezindua maabara mpya ambayo itatumika kwa kazi za kisayansi zitakazozisaidia nchi kushughulikia changamoto za chakula la kilimo. Jengo hilo lililozinduliwa nje kidogo ya mjini wa Vienna Austria ni hitimisho la ujenzi mkubwa wa mradi wa IAEA wa kukarabati maabara zake ziwe na ufanisi zaidi.

Maabara hiyo mpya iliyopewa jina la Flexibo Modular (FML) itakuwa maskani ya vitengo mbalimbali vya uchunguzi ikiwemo wa uzalishaji wa wanyama, afya, chakula na ulinzi wa mazingira, udhibiti wa udongo na maji na uzalishaji wa mazao.

Maabara hiyo iliyoko mjini Seibersdorf kilometa 40 kutoka mji mkuu Vienna ina maabara tatu kwa moja ambazo zitazisaidia nchi wanachama wa IAEA katika masuala ya utafiti na kuzijengea uwezo katika matumizi bora ya sayansi na teknolojia ya nyuklia.

Mbinu za nyuklia zinaweza kusaidia kuongeza uzalishaji wa mifugo, kubaini madahara na ubadhilifu katika chakula, kupambana na magonjwa yanayoweza kusambaa na kuboresha odongo na udhibiti wa maji miongoni mwa malengo  na mchango wa kufikia malengo ya maendeleo endelevu yaani SDG’s.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa IAEA Yukiya Amano ujenzi wa maabara hiyo ni mafanikio makubwa kwani “Ukarabati wa maaba hiyo na kuifanya ya kisasa ni moja ya mirani ya mara moja kwa nusu karne ambayo itaboresha huduma kwa kiasi kikubwa ambazo tutazitoa kwa nchi wanachama wetu 170.Pia itatusaidia katika kupigia upatu matumizi bora ya sanyansi na teknolojia ya nyuklia iliyoko duniani.”

Kwa mara ya kwanza maabara ya IAEA Seibersdorf ilifungua milango yake 1962 ikiwa na wafanyazi 40 na tangu wakati huo imepanua wigo wake na mahitaji ya huduma yameongezeka. Jengo hilo lenye maabara ndogondogo 8 hivi sasa lina wafanyakazi zaidi ya 200 na linafundisha wanasayansi zaidi ya 250 kutoka kote duniani kila mwaka.