Bado inawezekana kudhibiti ongezeko la joto chini ya 2°C

27 Novemba 2018

Ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP inasema bado inawezekana kudhibiti ongezeko la joto duniani kusalia chini ya nyuzi joto 2°C, lakini pengo la kiufundi la kuhakikisha dunia inagonga nyuzi joto 1.5°C linaongezeka.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya “pengo la uchafuzi wa mazingira 2018” kiwango cha kimataifa cha hewa chafuzi ya Cabon kimeongezeka mwaka 2017 baada ya kutofanya hivyo kwa miaka mitatu .

Kwa hivyo ripoti inasema endapo pengo hilo halitozibwa ifikapo mwaka 2030 basi itakuwa ni vigumu kufikia lengo la kuwa na nyuzi joto 2°C .

Sasa ripoti imezitaka nchi zote duniani kuongeza juhudi mara tatu kuhakikisha lengo hilo linatimia kwani uchafuzi wa hewa unaongezeka najuhudi z anchi kupambana na mabadiliko ya tabia nchi hazitoshelezi.

Kituo cha kusafisha mafuta Pancevo, Serbia kikipeleka uchafu angani
2001/2002 © UNEP
Kituo cha kusafisha mafuta Pancevo, Serbia kikipeleka uchafu angani

 

Matumaini ya kufikia malengo:

Hata hivyo ripori inasema vado kuna matumaini hasa kutokana na kasi ya sekta binafsi , uwezo wa ubunifu na ufadhili wa kuwa na uchumi unaochaji mazingira kwani vyote ni vichocheo vinavyotoa fursa ya kuziba pengo lililopo na linaloongezeka katika hewa chafuzi.

Ripoti hiyo ya kila mwaka ya UNEP inawasilisha tathimini ya kile kinachoelezwa kuwa ni “pengo la uchafuzi wa hewa” ambapo ni mlinganisho wa kiwango cha joto kinachotarajiwa ifikapo 2030 na kiwango halisi cha lengo la nyuzi joto 2°C / 1.5°C.

Wanyama kama huyu Dubu, kama ilivyo kwa viumbe wengine duniani, wanategemea kwa kiasi kikubwa hali ya joto la dunia kwa mstakabali wa maisha yao.
UNEP GRID Arendal/Peter Prokosch
Wanyama kama huyu Dubu, kama ilivyo kwa viumbe wengine duniani, wanategemea kwa kiasi kikubwa hali ya joto la dunia kwa mstakabali wa maisha yao.

 

Juhudi zinazohitajika:

Kwa mujibu wa ripoti hiyo pamoja na changamoto matokeo ya utafiti wa ripoti hiyo yanaonyesha kwamba juhudi za kitaifa na azma ya nchi nyingi ni kutimiza malengo ya mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi wa Paris. Ikiwa ni siku chache kabla ya mkutano wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi COP24, unaonyesha kwamba kiwango cha uchafuzi wa hewa kimataifa kimefikia khistoria ambapo katika nchi 57 kulikokusanywa takwimu kuna matumaini kwamba lengo litatimia ifikapo 2030 inagwa takwimu pia zinadhihirisha bayana kasi ya nchi kuchukua hatua haitoshelezi.

Hivyo wito umesisitizwa kwamba hatua dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi zinahitajika mara tatu zaidi kutoka kwa nchi zote kufikia lengo la kuwa na nyuzi joto chini ya 2°C na mara 5 zaidi kufikia lengo la nyuzi joto  1.5°C.

 

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter