Tunalaani vikali shambulio dhidi ya ubalozi wa China Karachi

24 Novemba 2018

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali shambulio la jana Novemba 23 dhidi ya ubalozi wa China mjini Karachi nchini Pakistan. Shambulio hilo limekatili maisha ya maafisa wawili wa polisi wa Pakistan na raia wawili.

Pia wajumbe hao wa Baraza wamelaani shambulio lingine la kigaidi lililotokea kwenye soko la Khyber jimbo la Pakhtunkhwa Pakistan siku hiyo hiyo na kuua watu takriban 35 na kujeruhi wengine wengi

Wajumbe hao wameshukuru hatua za haraka zilizochukuliwa na uongozi wa Pakistan na kutoa pole kwa familia za wafiwa na kuwatakia nafuu ya haraka majeruhi.

Wajumbe wa Baraza wamerejea kusisitiza kwamba mikataba yote ya kimataifa kuhusu diplomasia ni lazima iheshimiwe na kutekelezwa. Aidha wajumbe wameyahimiza mataifa yote kufanya kila liwezekenalo kupambana na ugaidi wa aina zote lakini pia  uchunguzi ufanyike na wahusika kuwajibishwa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter